Redds na Mwonekano Mpya

Image
Baada ya kuzindua kwa mafanikio mwonekano mpya wa Chupa ya Ndovu mwishoni mwa mwaka jana, Kampuni ya bia ya Tanzania Breweries imechukua hatua pana zaidi kuzindua mwonekano mpya wa chupa ya Redds Premium Apple Cider jioni ya Alhamisi tarehe 4 mwezi wa pili mwaka 2010..

Sherehe hiyo ya kuzindua mwonekano mpya wa kinywaji cha Redds ilihudhuriwa na watu wa madaraja mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa Mabenki, Kampuni za simu, wabunifu wa mitindo, waandishi wa habari na mamia ya wapenzi wa kinywaji hicho walioalikwa katika sherehe hiyo.

Image

Katika hotuba yake ya kuzindua mwonekano wa kinywaji hicho meneja wa kinywaji hicho bibie Kabula Nshimo alisema kinywaji hicho kilikuwa kwenye chupa ya ujazo wa mililita 330 na sasa inapatikana kwenye chupa ya mili lita 375 ambayo inarudishwa baada ya kunywa. Tumechukua hatua hii kama sehemu ya kuwaonyesha wateja wetu ni kiasi gani tunawajali. Hichi ni kinywaji cha kwanza ambacho ukinywa unapata kujiamini na kuonekana mjanja, pia kinywaji hichi kinaenzi urembo wa mwafrika.

Image

Akiongea machache katika Hafla hiyo mkurugenzi wa masoko katika kampuni hiyo bwana David Minja alisema Kampuni ya TBL imekuwa ikijitahidi kuwa mstari wa mbele katika kuendana na mabadiliko ya kisoko hivyo uzinduzi wa mwonekano mpya wa kinywaji cha Redds ni mwendelezo wa mabadiliko hayo.

Image

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya TBL bwana Robin Goetzsche akiongea na waageni waalikwa alisema Redds ni moja kati ya vinywaji maarufu vya matunda vyenye kilevi, hivyo mwonekano mpya wa chupa ya kinywaji hicho utahakikisha kinywaji hicho kinabakia maarufu kwa wapenzi wa sasa na wapya wanaotegemewa kuanza kukitumia kinywaji hichi baada ya maboresho haya.

Image

Ikumbukwe kinywaji cha Redds Premium Apple Cider kimekuwa kikijihusisha na tasnia ya ubunifu wa mavazi ambako ndio chimbuko la wengi wa warembo wanaoshiriki katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Tanzania ambapo Redds imekuwa mdhamini shiriki ama mwenza katika ngazi ya vitongoji na kanda.

Bongo5 inapenda kuwapongeza TBL na kinywaji cha Redds kwa ubunifu wao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents