Habari

Redio za jamii msitumiwe na Wanasiasa – Mhe. Wambura

Redio za jamii nchini zimeshauriwa kutotumiwa na wanasiasa katika uendeshaji wa kazi zao bali zizingatie dhumuni kuu la kuelimisha wanajamii katika kuleta maendeleo ya Jamii.

Hayo yamesemwa na leo Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe, Anastazia Wambura alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo yahusuyo Radio ya Jamii kwa Maendeleo Vijijini kwa waandishi wa habari, wawakilishi kutoka Halmashauri za Wilaya nchini yaliyofanyika Mjini Dodoma.

Mhe. Wambura amesema kuwa Redio za Jamii zinatakiwa kusimamia malengo yao makuu ya kuwa karibu na jamii husika na kuzifanya jamii hizo kunufaika na Redio hizo na sio kufarakanisha jamii.

“Nisistizie kwa washiriki kuzingatia malengo ya mafunzo haya mnayopewa ili yasaidie katika kuielimisha jamii katika masuala mbalimbali na kuachana na masuala ya siasa,” alisistiza Mhe. Anastazia.

Mhe. Anastazia Wambura amesisitiza kuwa wataalamu wa habari wanatakiwa kutumiwa vizuri katika Halmasahuri nchini ili kuzisaidia Redio za Jamii ziweze kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi.

Waandishi wa habari kutoka katika Redio za jamii nchini pamoja na wawakilishi kutoka Hamlashauri za Wilaya nchini wapo katoika mafunzo ya siku mbili yahusuyo Radio ya Jamii kwa Maendeleo Vijijini yanayofanyika Mjini Dodoma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents