Burudani
Redsan amshirikisha AY kwenye ngoma mpya
AY na Redsan wameingia studio kurekodi wimbo pamoja.
Ni wimbo wa Redsan aliomshirikisha rapper huyo mkongwe wa Tanzania.
Wawili hao jana usiku walikuwa ndani ya studio za Sappy Music Lab iliyo chini ya producer wa Tanzania aishiye nchini Kenya, Sappy. AY na Sappy wamepost picha zao wakiwa studio.
Sappy na AY
“Thanks my bro for coming through…Umekill Verses…@redsanmusic Ft @Aytanzania.- SappyMusicLab,” ameandika Sappy.
Naye AY amepost picha na kuandika: Studio Flow na Wazee wa Kazi @redsanmusic & @dr_sappy #GoodMusic #Cookin #SappyMusicClub #Madaktari.”