Michezo

Refa aliyetoa kadi nyekundu kimakosa kwenye mechi ya Arsenal na Chelsea aomba radhi

Refa Andre Marriner huenda akawekwa kando kwenye michezo ya mwishoni mwa juma baada ya kufanya makosa yakutoa kadi nyekundu kwa mchezaji wa kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Arsenal na Chelsea ambapo Chelsea ilishinda 6 bila.

kieran-gibbs-getty_2860195b

Marriner alitoa Penalti wakati wa mchezo wa siku ya Jumamosi baada ya Alex Oxlade-Chamberlain kushika mpira, lakini Kieran Gibbs alipewa kadi nyekundu na kuondolewa kimakosa. Oxlade-Chamberlain alionekana akimwambia Refa kuwa yeye ndiye aliyeshika mpira, hata hivyo uamuzi wa awali ndio ulikua wa mwisho.

Hata hivyo baadaye Mariner alikiri na kuomba radhi kwa makosa yaliyojitokeza, akikiri kufanya makosa kutomtambua aliyepaswa kuadhibiwa katika mchezo huo. Chama cha waamuzi wa mchezo wa kulipwa kimesema kuwa matukio ya kumwadhibu mchezaji kimamkosa ni nadra kutokea na mara nyingi husababishwa na sababu mbalimbali za kiufundi

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents