Habari

Reginald Mengi atia neno uchaguzi wa urais Kenya

By  | 

Macho ya watu wengi kwa sasa yameelekezwa katika uchaguzi mkuu wa nchini Kenya ambao unatarajiwa kufanyika wiki ijayo ya August 8.

Mfanyabiashara maarufu na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Limited, Dkt. Reginald Mengi amekuwa miongoni mwa watu wakubwa ambao wanafuatilia kwa ukaribu uchaguzi huo huku akiombea upite kwa amani tofauti na ule uliotokea miaka minne iliyopita.

Mengi amethibitisha hilo kupitia mtandao wake wa Twitter kwa kuandika, “This is a historical election for Kenya. A peaceful election is victory not just for Kenyans but all East [email protected] @RailaOdinga.”

Katika uchaguzi huo vita kubwa ya kuwania kiti cha urais ipo kwa Uhuru Kenyatta ambaye anawakilisha chama cha Jubilee Party na Raila Odinga ambaye anawania kupitia umoja wa NASA.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments