Fahamu

Rekodi mbovu na mkosi wa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, kushindwa katika mchezo wa fainali, fahamu fainali alizoshindwa

Rekodi mbovu na mkosi wa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, kushindwa katika mchezo wa fainali, fahamu fainali alizoshindwa

Rekodi ya Jurgen Klopp ya kufikisha timu yake katika fainali hi ya kupigiwa mfano- lakini kiwango cha ufanisi wake ni cha kuvunja moyo. Kocha wa Liverpool anaelekea katika fainali ya ligi ya mabingwa ya siku ya Jumamosi dhidi ya Tottenham akiwa na mkosi kushindwa katika fainali sita mfululizi. Mbili kati ya mkosi huo ni kushindwa katika fainali ya ubingwa wa Ulaya – Kwa hiyo wikendi hii Mjerumani huyo anapania kujiepusha na kosa lolote litakalo mkumbusha makovu yaliyopita .

Hili ni taji la 8 kubwa kwa kocha huyo wa miaka 51 na la 4 kwa msimu wake wa tatu katika klabu ya Liverpool.

BBC Michezo inafuatilia kwa karibu jinsi timu ya Klopp ilivyofanya katika mataji makubwa yaliyopita

Mei 12 2012: Fainali ya Michuanio ya Kombe la Ujerumani – Borussia Dortmund 5-2 Bayern Munich, Olympic Stadium, Berlin

Ilianza vyema kwa Klopp.

Baada ya kushinda mataji mawili ya Bundesliga akiwa na Borussia Dortmund, aliishindia klabu hiyo taji la tatu la michuano ya kombe la Ujerumani baada ya kuirarua Bayern Munich mjini Berlin chini ya Jupp Heynckes.

Robert Lewandowski, ambaye baadae alihamia Bayern, alifunga hat-trick huku mabao mengine ya Dortmund yakifungwa na Shinji Kagawa, ambaye baadae alihamia Manchester United, na Mats Hummels, ambaye pia alijiunga na miamba wa Munich.

“Huo ilikuwa ushindi ambayo hakuna hata mtu mmoja wa Dortmund alitegemea,” ulikuwa mchezo wa kusisismua alisema Klopp. “Ni vigumu kuelezea tulishikwa na nini.”

Lilikuwa taji la kwanza la Ujerumani kwa Dortmund kunyakua baada ya kutawazwa washindi wa ubingwa wa Ulaya baada ya kushinda kwa paointi nane mbele ya Bayern.

“Ushindi huo wa mara mbili ulikuwa kitu kizuri sana kwangu,” aliongeza Klopp.

Kuvunjwa moyo dakika za mwisho mwisho Wembley

Mei 252013: Fainali ya Ubingwa wa Ulaya – Borussia Dortmund 1-2 Bayern Munich, Wembley.

Baada ya kufanya vizuri dhidi ya Real Madrid chini ya Jose Mourinho wakati huo na kupata tiketi ya nafasi ya nne bora, kutinga fainali ya Ubingwa wa Ulaya katika miaka 16, Dortmund walielekea Wembley wakiwa na matumaini ya kunyakuwa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya pili.

“Watu washajaribu kukwea mlima Everest na kuamua kurudi wakiwa wamesalia na mita 10 kufika kileleni,” alisema Klopp kuelekea fainali dhidi ya Bayern Munich ambayo iliyohusisha timu mbili za Ujerumani .

Lakini mchuano huo wa kusisimua uliishia kilio kwa Klopp na Die Schwarz-Gelben baada ya Arjan Robben kufunga bao katika dakika ya 89 na baada ya penati ya Ilkay Gundogan kufuta bao la ufunguzi la Mario Mandzukic wa Bayern.

“Ulikuwa msimu mgumo sana kwetu na niliona hilo kuanzia dakika ya 75,” Klopp alisema baadae.

“Tulistahili kufika fainali. Hilo sio jambo muhimu, lakini ni muhimu.”

Guardiola aliibuka na ushindi dhidi ya Klopp

Mei 17 2014: Fainali ya Kombe la Ujerumani – Borussia Dortmund 0-2 Bayern Munich, Olympic Stadium, Berlin

Ulikuwa msimu mwingine, fainali nyingine – ambayo iliwakutanisha tena Dortmond na Bayern Munich. Wakati huo hatahivyo kulikuwa na tofauti.

Japo Heynckes alikuwa mkufunzi wa Bayern katika fainali mbili zilizopita, wakati huo ilikwa Pep Guardiola ndiye alikutana na Klopp katika fainaliya Kombe la Ujerumani mwaka 2014.

Jurgen KloppHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionJurgen Klopp ilikuwa mkufunzi wa Borussia Dortmund, kwa misimu saba na alishinda mataji mawili ya Bundesliga moja ya Ujerumani na moja ya Ubingwa wa Ulaya

Mshambuliaji wa Dortmund Robert Lewandowski, ambaye alikuwa amkubali kuhamia Munich mwisho wa msimu aliondolewa katika baadhi ya mazoezi kabla ya fainali kama sehemu ya kumkinga asiumizwe.

“Tulikuwa makini sana,” alisema Klopp kabla ya mchezo.

Tofauti na fainalizingine za Ubingwa wa Ulaya miezi 12 ya awali, timu ya Klopp walijitahidi kufika muda wa ziada kabla ya magoli ya Robben na Thomas Muller.

“Ilikuwa uchungu sana kwetu kwasababu lilikuwa shindano kubwa. Timu zote mbili zilijitahidi kuliko kifani,” alisema baadae.

Kweheri ya Klopp kutoka Dortmund– Alishindwa

Mei 30 2015: Fainali ya Kombe la Ujerumani – Borussia Dortmund 1-3 Wolfsburg, Olympic Stadium, Berlin

Hii ilikuwa mechi ya mwisho ya Klopp, Dortmund bada ya kuwa mkufunzi wa klabu hiyo kwa miaka saba.

Tayari alikuwa ametangaza uamuzi wa kuondoka baada ya kibarua kigumu kwa Dortmund iliyoishia kumaliza katika nafasi ya saba licha ya kuwa chini ya jeduali la ligi hiyo mwezi Februari.

“Klabu hii inahitaji kuongozwa na meneja ambaye anajitolea kwa 100%. Sio kwamba nimechoka. Nataka kufanya kazi na vilabu vingine.” alisema baadae.

Kazi ya mwisho ya Klopp akiwa Dortmund ilikuwa mchezo wa fainali uliomalizika kwa machungu zaidi – Kevin de Bruyne ambaye sasa yuko Manchester City alikuwa miongoni mwa wafungaji waliyoifanya Wolfsburg kutoka nyuma na kunyakuwa ushindi wa Kombe la Ujerumani baada ya kufunga mabao matatu katika dakika 16 za mwanzo wa kipindi cha kwanza.

“Nahitaji muda kukabiliana na hali hii,” alisema Klopp, kabla ya kuipungia mkono Dortmund.

Jurgen Klopp applauds on the sidelines during Borussia Dortmund's 2015 German Cup final defeat by WolfsburgHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionThe 2015 German Cup final was Jurgen Klopp’s final game in charge of Borussia Dortmund

Februari 28 2016: Fainali ya kombe la ligi ya England – Liverpool 1-1 Man City (Man City ilishinda 3-1 ), Wembley

Miezi minne ebaada ya kuchukua nafasi ya Brendan Rodger, Liverpool, na miaka mitatu baada ya kushindwa Ubingwa wa Ulaya akiwa Dortmund katika London stadium, Klopp alirejea tena Wembley kwa fainali nyingine.

Matokeo hayakuwa tofauti na vile ilivyotarajiwa kwa kocha huyo wa Reds’.

Willy Caballero aliokoa penati za Lucas Leiva, Philippe Coutinho na Adam Lallana kumshindia Kombe la Ligi kocha Manuel Pellegrini wa Manchester City baada ya kutoka sare ya 1-1 ambapo mshindi aliamuliwa kupitia penati.

“Tunajihisi wanyonge lakini lazima tusimame kidete. Ni mtu mjinga tu ndiye atakayesalia sakafuni na kusubiri kushindwa tena,” alisema Klopp baadae.

Kipa Willy Caballero aliokoa penati tatuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKipa Willy Caballero aliokoa penati tatu

Nakiri makosa

Mei 18 May 2016: Fainali ya ligi ya Europa – Liverpool 1-3 Sevilla, St Jakob-Park, Basel

Miezi mitatu baada ya kushindwa taji la ligi Kuu, Liverpool walitinga fainali ya ligi yaEuropa League baada ya kinyang’anyiro kilichohusisha ushindi wa 5-4 dhidi ya klabu ya zamani ya Klopp Borussia Dortmund katika robo fainali.

Ilionekena Mjerumani huyo ataepuka mkosi wa kushindwa katika fainali imefikia kikomo baada ya Daniel Sturridge kuiweka Liverpool kifua mbele dhidi ya Sevill ya Unai Emery nchini Switzerland.

Lakini ndoto hiyo ilizimwa baada ya miamba hao wa Uhispania kushinda taji hilo kwa msimu wa tatu mfululizo na kuiondoa Livepool katika michuano ya Champions League.

“Hii ingelikuwa ushindi wa 4-1 au 5-1 lakini Liverpool ilipoteza,” mlinzi wa Reds Mark Lawrenson aliiambia on BBC Radio 5 Live.

Klopp alikubali matokeo na kuwaambia mashabiki kumlaumu yeye, akiongeza kuwa: “Hakuna haja ya kuwalaumu wachezaji nimesema nao.”

Mei 26 2018: Finali ya Champions League – Real Madrid 3-1 Liverpool, Olympic Stadium, Kiev

Gareth Bale alifunga moja ya bao kali zaidi katika soka ya Ulaya huku kipa wa Liverpool Loris Karius ambaye alimsababishia pigo Klopp pigo la kupoteza taji kuu nyingine kwa mara ya sita

The Reds tayari walikuwa wanakosa huduma ya mshambuliaji Mohamed Salah walipambana kiasi cha haja ambapo Sadio Mane alifunga bao la kusawazisha.

Lakini Bale aliingia na kufunga cao lingine la kushangaza kabla ya kuongeza lingine lililoipatia ushindi Real.

Liverpool goalkeeper Loris Karius in action during the 2018 Champions League finalHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKipa wa Liverpool Loris Karius

“Mpango wetu ulikuwa kucheza na kushinda na wala sio lingine,” alisema Klopp, amabye baadae alimtuma Kipa Karius kwenda Besiktas ya Uturuki kwa mkopo wa miaka miwili.

Miezi 12 baadae, na baada ya kutolewa tonge mdomoni na Manchester City katika kinyang’anyiro cha fainali ya ligi ya Premier, Liverpool wanarejea tena kuasaka Ubingwa wa Ulaya kufuatia nusu fainali ya kusisimua dhidi ya Barcelona na kutinga fainali.

Je Klopp atavunja mkosi wa kushindwa katika fainali… au atakubali kushindwa kwa mara ya saba mfululizo?

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents