Michezo

Rekodi za kutisha za Usain Bolt hizi hapa

Usain St Leo Bolt anakubalika kuwa mwanariadha mashuhuri wa mbio fupi duniani. Huku raia huyo wa Jamaica akijitayarisha kustaafu baada ya mashindano ya dunia mjini London hizi hapa sababu 9.58 kwa nini anafaa kuitwa shupavu na vile alivyoweza kupata ufanisi huo.

1.Ndiye mwanariadha anayeweza kukimbia kwa kasi ya juu katika historia.

Bolt amevunja rekodi tatu za dunia katika mita 100 na ni miaka tisa tangu alipovunja rekodi ya kwanza.

Bolt alivunja rekodi iliowekwa na mwenzake wa Jamaica Asafa Powell ya 9.74 akiweka muda wa 9.72 mnamo mwezi Mei 2008 na kuivunja tena rekodi hiyo hadi 9.69 katika michezo ya Olimpiki ya Beijing.

Katika riadha za dunia za 2009 mjini Berlin alivunja tena rekodi hiyo kwa kuweka muda wa 9.58.

Mwaka 1912, mwanariadha wa Marekani Donald Lippincott alikimbia muda wa sekunde 10.6 mjini Stockholm hivyobasi kuweka muda bora uliotambulika na shirikisho la riadha duniani IAAF.

Jim Hines mwaka 1969 alikuwa mtu wa kwanza kushusha muda wa sekunde 10 , lakini ilichukua karibu karne nzima kwa muda huo wa Lippincott kuvunjwa kwa sekunde moja kupitia Usain Bolt.

2.Amekimbia kwa kasi kila mara.

Orodha ya wanariadha wote wa mita 100 inayomilikiwa na I.A.A.F inaonyesha kuwa ni wanariadha wachache pekee waliokaribia muda uliowekwa na Bolt.

Kila mita 100 chini ya sekunde 10

Tangu wakati wa Hines watu wengine 124 waliweza kukimbia chini ya muda wa sekunde 10.

Lakini hakuna hata mtu mmoja isipokuwa Bolt , mwenzake wa Jamaica Yohan Blake na Asafa Powell pamoja na Wamarekani Justin Gatlin na Tyson Gay waliokimbia chini ya sekunde 9.78.

Bolt pekee amefanikiwa kukimbia chini ya muda huo mara tisa.

3.Na sio mita 100 pekee.

Bolt amefanikiwa katika mbio za mita 200 na ni mwanariadha wa kipekee kumiliki rekodi za dunia katika mbio mbili tangu IAAF ilipoanza kuweka muda wa kiteknolojia 1977.

Walioshikilia rekodi za dunia mita 100 na 200 tangu 1997

Katika mashindano ya Olimpiki ya 2008 mjini Beijing, Bolt alivunja rekodi ya dunia ya miaka 12 iliowekwa na Michael Johnson ya sekunde 19.32 kwa kuweka muda wa sekunde 19.30 kabla ya kuivunja tena rekodi hiyo kwa muda wa sekunde 19.19 mwaka mmoja baadaye mjini Berlin.

4.Amekuwa akishinda kila mara.

Mbali na mashindano ya riadha mjini London, Bolt amefanikiwa kupata ushindi katika kila michezo ya Olimpiki na ile ya dunia tangu 2008.

Mjini Rio 2016, alifanikiwa kushinda medali za dhahabu katika mbio za mita 100, 200 na 4x100m relay na kumfanya kuwa ”asiyewezekana”.

Dhahabu zilizozolewa na bolt katika maisha yake ya riadha

 

Bolt hatahivyo alipokonywa taji la relay la 2008 baada ya mwenzake Nesta Carter kutambulika kwamba alitumia dawa za kusisimua misuli hatua ilioathiri kundi lote la relay.

Hatahivyo Carter amekata rufaa na mahakama ya kutatua maswala ya michezo.

Hatahivyo ubingwa wa dunia wa Bolt ulikamilika kwa kujipatia medali ya shaba mjini London 2017 mbali na kuanza vibaya katika mbio za mita 100 mjini Daegu Korea Kusini 2011 ambapo alipigwa marufuku.

5.Alishindwa mara moja 2008.

Ni wanariadha gani waliomshinda Bolt

Kutoka 2008 hadi kufikia sasa alishindwa mara moja katika mbio za mita 200 na mwenzake wa Jamaica Yohan Blake katika mbio za kitaifa za Jamaica 2012.

Blake pia alishinda mbio za mita 100 katika mashindano hayo, ikiwa ni mojawapo ya mbio ambazo Bolt alishindwa kutamba katika mashindano muhimu.

Gatlin ,Christian Coleman, Powell na Gay ni wanariadha wengine walioweza kumshinda Bolt katika mbio za mita 100

6.Ana kasi zaidi ya unavyodhania.

Bolt alikimbia kwa kasi katika mbio za mita 10 za mita 100 katika rekodi ya dunia ya sekunde 0.81. Hiyo ni sawa na kilomita 44.51 kwa saa kasi sawa na ile ya farasi

 

Bolt akishindana na wanyama na baiskeli

Lakini raia huyo wa Jamaica ameweza kukimbia mita 100 kwa kasi zaidi ya muda wa sekunde 9.58 alipoanza kwa kukimbia .

Alikimbia nusu ya sekunde 19.19 za mita 200 kwa sekunde 9.26 na ameweka muda mzuri wa chini ya sekunde tisa mara kadhaa katika mbio za 4x100m relay huku muda bora ukiwa wa sekunde 8.65 mwaka 2015.

Hatahivyo miaka na majeraha yamemuathiri Bolt ambaye anakaribia kuwa na miaka 31. Muda bora alioweka msimu huu umepungua na hajakuwa akikimbia mara kwa mara.

Mwaka 2016 alikimbia mita 100 kwa muda wa sekunde 9.81 na 19.78 katika mbio za mita 200 ikiwa ni muda wa chini lakini akaibuka mshindi.

7.Je yeye hufanyaje?

Hakuna jibu la rahisi lakini utafiti uliofanywa na Mackala Krzysztof na Antti Mero uliochapishwa katika jarida la mwendo wa binadamu ulibaini kwamba urefu wake wa futi 6 nchi 5 ni mojawapo ya sababu ambazo zinampa uwezo mkubwa dhidi ya wenzake.

Urefu wake wa futi 6 nchi 5 ni mojawapo ya sababu ambazo zinampa uwezo mkubwa dhidi ya wenzake.

Urefu unampatia mwanariadha huyo fursa kubwa wakati wa kuanza kwa mbio ikilinganishwa na wanariadha wengine wakati wanapoanza kukimbia.

lakini watafiti wanasema kufikia katikati urefu wa Bolt kutokana na misamba yake mirefu unamwezesha kuwa na kasi ya juu kwa muda mrefu na kupunguza mwendo ikilinganishwa na wanariadha wafupi.

8.Na urefu wa misamba yake ni wa mita 2.47.

Ukiwa ni sentimita 20 zaidi ikilinganishwa na wanariadha wengine.

Misamba ya Bolt ni mirefu ikilinganisha na wanariadha wengine

Ni mchanganyiko wenye uwezo mkubwa ikilinganishwa na wakimbiaji wengine kwa kuwa wakati anapochanganya mbio anaweza kusonga mbele kwa haraka.

Raia huyo wa Jamaica alikimbia mita 100 kwa kupiga misamba 41, huku wanariadha wengine wakipiga misamba 45 ,kulingana na Krzysztof na Mero found.

9.Na inakuwaje wanariadha warefu huenza mbio kwa kujikokota?

Ijapokuwa Bolt mara kwa mara hufanikiwa kuimarisha kasi yake baadaye

Ni kweli kwamba hujikokota anapoanza mbio ikilinganishwa na wanariadha wengine. Unapochunguza wakati wake wote anapoanza mbio za Olimpiki na zile za ubingwa isipokuwa zile za Daegu alikokosea na kupigwa marufuku kuendelea 2011 ana wastani wa sekunde 0.158 huku wengine wakiwa na wastani wa sekunde 0.149

Bolt hujikokota anapoanza mbio

Lakini kulingana na Michael Johnson, katika mbio zake alizokimbia vyema, Bolt alifanikiwa kukimbia sawa na wanariadha wasio warefu.

Utaona kwamba katika mita 30 za kwanza yuko sawa na wanariadha wengine wasio warefu ambalo sio jambo la kawaida.

katika mbio alizovunja rekodi ya dunia, Bolt alikuwa na kasi katika mbio zote.

Alikuwa mbele mita 20 za kwanza na kuendelea hivyohivyo katika kila mita 20 zilizosalia.

Mjini London 2017, hatahivyo muda wake ulikuwa wa chini ikilinganishwa na wanariadha wote katika mbio hiyo.

9.58 Bolt ana umaarufu mwengine.

Mbali na kasi ‘yake ya umeme’, na mapozi yake katika uwanja anadai kula vipande 1000 vya kuku katika mashindano ya Olimpiki ya Beijing, utani wake binafsi umempatia umaarufu.

Kujigamba kwake kabla ya kuvuka utepe hakujamuharibia sifa yake miongoni mwa mashabiki.

Siku moja kabla ya kutangaza kustaafu kwake, ni mwanariadha aliye na umaarufu mkubwa katika mitandao ya kijamii akiwa na ufuasi wa watu milioni 19 katika facebook, milioni 7.1 katika Instagram na milioni 4.75 katika mtandao wa Twitter.

Mashabiki wa Bolt katika mitandao ya kijamii

Mbali na umaarufu kuna ufadhili. Ametia kandarasi na Puma, Mumm champagne, Advil na wengine kumpatia mapato ya kila mwaka ya dola milioni 34.2 katika kipindi cha mwaka 2016-17 kulingana na jarida la Forbes ambalo linamuorodhesha miongoni watu wake 100 walio maarufu.

Bolt huwasaidia wasiojiweza kupitia wakfu wake ikiwemo kusaidia shule yake ya zamani huko Trelawny Parish, Jamaica.

lakini je atajiondoa katika ulimwengu wa umaarufu na kujificha katika kivuli? Bolt mwenyewe anasema kuwa anataka kupumzika kiasi na kujivinjari kwa kiasi kikubwa.

Na baada ya hilo pengine ataendelea kujihusisha na riadha ya dunia.

Lakini hakuna tashwishi kwamba mchezo huo utamkosa. Mwenyekiti wa IAAF Lord Coe aliambia BBC hivi majuzi: Kile tutakachokosa ni ule utu. Tunapenda wanariadha wenye utu.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents