Bizzare

Rekodi za Kylie Jenner na Justin Bieber zavunjwa ‘kimazingaombwe’ kwenye mtandao wa Instagram

Ukizungumzia kwa sasa posti ambayo ina likes nyingi kwenye mtandao wa Instagram kwa sasa basi ni posti ya picha ya yai na sio posti za picha ya mrembo Kylie Jenner na Justin Bieber tena.

https://www.instagram.com/p/BsOGulcndj-/

Picha hiyo ya Yai ambayo imepostiwa Januari 4, 2019 mpaka sasa ina likes milioni 38.8 na ndio inakuwa posti ya kwanza kuwa na likes nyingi duniani kwenye mtandao wa Instagram ikifuatiwa na posti ya Kylie Jenner aliyomposti mtoto wake yenye likes milioni 18.5 .

https://www.instagram.com/p/Be3rTNplCHf/?utm_source=ig_embed

Posti ya msanii wa muziki kutoka Canada, Justin Bieber inashika nafasi ya tatu ikiwa na likes milioni 13 na ilichapishwa kwenye mtandao huo pendwa duniani July 9, 2018 .

Ingawaje bado haijafahamika ni nani anayeendesha ukurasa huo wa yai, lakini mtandao wa Washington Post umeleeza kuwa umefanikiwa kumpata mtu aliyefungua akaunti hiyo ya ‘EGG GANG’, ambapo umeandika kuwa mtu huyo anaishi London, Uingereza na alifungua akaunti hiyo Januari 4, 2018 .

Mtandao huo umesema jamaa huyo, alifanya hivyo baada ya kutafuta mtandaoni picha yenye likes nyingi kwenye mtandao wa Instagram.

Hapa chini ni orodha ya posti zenye likes nyingi kwenye mtandao wa Instagram duniani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents