Michezo

Rekodi za vilabu vya Uhispania vilivyotawala soka barani Ulaya ndani ya miaka 10

Rekodi za vilabu vya Uhispania vilivyotawala soka barani Ulaya ndani ya miaka 10

Vilabu vya Uhispania vimeendeleza ubabe wao katika michuano mikubwa barani Ulaya,kwa kuendelea kufanya vizuri na kuifanya ligi ya Uhispania Iendelee kuonekana ni ligi bora Duniani.

Hii inatokana na kwamba bado hakuna ligi yenye upinzani kwa ligi ya Uhispania alimaarufu Laliga,hasa katika vilabu vinavyopata nafasi ya kushiriki michuano mikubwa.

Ikumbukwe kuwa klabu ya Real Madrid ndio inayoongoza barani Ulaya kwa kutwaa taji la UEFA Champions League ikitwaa taji hili mara 13,huku katika michuano ya UEFA Super Cup ikiongoza klabu ya FC Barcelona ikitwaa taji hili mara 5,lakini pia katika michuano ya UEFA Europa League klabu kutoka Uhispania ambayo ni Sevilla ndio inayoongoza kutwaa taji hili ikitwaa mara 5.

lakini pia katika michuano yote hii mitatu ambayo ni UEFA Champions League,UEFA Super Cup,UEFA Europa League,mataji yote haya yakiwa mikononi mwa vilabu vya Uhispania,UEFA Champions League ikiwa mikononi mwa Real Madrid,UEFA Europa League likiwa mikononi mwa Atletico Madrid na UEFA Super Cup likiwa mikononi mwa Atletico Madrid pia.

Licha ya vilabu hivyo kuendelea kufanya vizuri katika michuano hiyo lakini ndio vilabu vinavyoongoza kutwaa mataji haya ndani ya miaka 10,kuanzia mwaka 2009-2018 kwani ndani ya miaka 10 wakishinda mara 9.ifuatayo ni rekodi ya vilabu vilivyotoa taji hili la UEFA Super Cup kuanzia mwaka 2009.

2009 – Barcelona

2010 – Atletico Madrid

2011 – Barcelona

2012 – Atletico Madrid

2013 – Bayern Munich

2014 – Real Madrid

2015 – Barcelona

2016 – Real Madrid

2017 – Real Madrid

2018 – Atletico Madrid

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents