Habari

Reli ya Tanga hadi Arusha kutumika April mwakani

Serikali imeanza kufufua reli ya kutoka Tanga hadi Arusha iliyokufa miaka 14 iliyopita ili kuwezesha wafanyabiashara na wananchi kusafirisha mizigo yao kwa kutumia reli hiyo badala ya barabara.

Amesema hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wakati alipokagua ukarabati wa reli hiyo kuanzia eneo la Korogwe hadi Mombo ambalo limekamilika kwa KM 83 na kuwahikikishia watanzania kuwa uendelezaji wa reli hiyo hadi Arusha itakamilika mapema mwezi Aprili mwakani.

“Niwahakikishie wananchi kuwa hii kazi tuliyoianza haiwezi kusimama kwani Serikali imejipanga na itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri za usafirishaji” amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa, amemtaka Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za reli (RAHCO), Masanja Kadogosa, kuongeza ajira kwa vijana wa maeneo hayo na kuwataka kuwa na uzalendo katika ukarabati wa reli hiyo ili kurahisisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Aidha Prof. Mbarawa amezungumzia umuhimu wa kuongeza vichwa vya treni kwa Shirika hilo ambapo Serikali imeamua kununua vichwa 11 vya treni vilivyotelekezwa eneo la Bandari ya Dar es Salaam kwa kiasi cha shilingi dola milion 2.4 kutoka dola milion 3.2.

“Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa kila fedha inayopatikana itasimamiwa na kuwekeza katika miundombinu ya nchi na zaidi tumeokoa dola laki nane sawa na bilioni 1.7 kwa kila kichwa” amesisitiza Waziri Mbarawa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents