Michezo

Renato Sanches ashinda tuzo ya mchezaji chipukizi Euro 2016

Mchezaji kinda Renato Sanches ametajwa kuwa mchezaji bora kijana wa fainali za Ulaya (Euro 2016) ambazo zilifikia tamati usiku wa kuamkia hii leo jijini Paris nchini Ufaransa.

Renato-Sanches

Kiungo huyo ambaye ni kinda akatika michuano hiyo ya (Euro 2016) ameshinda tuzo hiyo na kuwashinda wenzake Kingsley Coman wa Ufaransa na Mreno mwenzie Raphael Guerreiro.

Zawadi hizo ambazo zilikuwa maalum kwa wale wote waliozaliwa baada ya January 1 1994, zilitolewa na jopo la Wataalamu wa masuala ya Kiufundi wa UEFA lililokuwa likiongozwa na Lupescu. Wengine waliokuwa kwenye jopo hilo ni Sir Alex Ferguson na Alain Giresse.

Sanches alianza kuonesha uwezo wake pale tu alipopewa nafasi kwenye mchezo dhidi ya Poland na kuonesha kiwango bora kabisa kilichomshawishi kocha wake kumuanzisha kwenye mechi zilizofuata.

Sanches alifunga goli lake la kwanza kwa timu yake katika mchezo dhidi ya Poland na kumfanya kuwa mchezaji wa tatu kijana kucheza mchezo wa fainali ya Euro mwaka huu.

Alikuwepo kwenye michezo yote muhimu ambayo Ureno walipata ushindi, ambayo ni dhidi ya Wales ambapo walishinda 2-0 na jana dhidi ya Ufaransa na kumfanya kushinda tuzo hiyo katika umri mdogo zaidi wa miaka 18 na siku 328.

Kinda huyo mzaliwa wa Lisbon, ambaye kwenye dirisha hili la usajili amejiunga na FC Bayern München akitokea Benfica kwa ada ya awali ya uero milioni 35, alianza msimu wa 2015/16 akiwa na timu B ya Benfica na kushiriki katika Michuano ya Ligi ya Vijana ya UEFA, Michezo ya kufuzu Michuano ya Ulaya kwa vijana chini ya miaka 19 na vile vile Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kupata nafasi ya kucheza timu ya taifa ya Ureno kwa mara ya kwanza Machi 25 mwaka huu.

Renato Sanches na Kingsley Coman msimu ujao watakuwa wote kwenye klabu ya Bayern huku Raphael Guerreiro naye atakuwa katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents