Rest In Peace Balali

Aliyekuwa gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Daudi Balali amefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita huko nyumbani kwake, Washington DC, nchini Marekani

Daudi Balali

 

 

 

Aliyekuwa gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Daudi Balali amefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita huko nyumbani kwake, Washington DC, nchini Marekani.

 

Habari kutoka kwenye vyanzo tofauti vya habari nchini, zinathibitisha ya kwamba Balali amefariki na sasa wapo kwenye maandalizi ya mazishi ambayo yanatarajiwa kufanyika siku ya ijumaa nchini humo.

 

Taarifa zaidi zinabainisha ya kwamba, familia ya marehemu Balali imeshaitaarifu serikali kutokana na kifo hiko na serikali inatarajia kutangaza rasmi habari hizo leo.

 

Ndugu mmoja alipoulizwa na chanzo kimoja cha habari nchini kwanini hakuweza kutoa taarifa hizo mapema alisema ya kwamba walihitajika kufanya hivyo ili waweze kupata fursa ya kuwasiliana na serikali pamoja na ndugu wengine na ndipo waweze kutangaza rasmi.

 

Kifo cha gavana huyo wa zamani bado hakijajulikana ila wana wasiwasi mkubwa na kifo hicho kwani bado hawaelewi ni kitu gani kilichosababisha msiba huo.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents