Rest In Peace Mwajuma

Meil JNIAKama itakumbukwa mnamo tarehe 2/4 wanafamilia wa bongo5 walipoteza moja wa wanachama wao aliyefariki huko Leeds nchini Uingereza, taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka uingereza zimefanyika kwa ushirikiano wa ndugu na jamaa wa marehemu

MWAJUMA IBRAHM SEIF


 


Kama itakumbukwa mnamo tarehe 2/4 wanafamilia wa bongo5 walipoteza moja wa wanachama wao aliyefariki huko Leeds nchini Uingereza mwenye jina la MWAJUMA IBRAHM SEIF, taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka uingereza zimefanyika kwa ushirikiano wa ndugu na jamaa wa marehemu walioko Leeds na Tanzania.



Mwili wa marehemu mwajuma umeiwasili jana uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere mnamo saa tisa na nusu jioni kwa shirika la ndege la Emirates ukitokea uingereza na kupokelewa na watu wengi waliofurika uwanjani wakisubiri, huku wengi wao wakiwa na simanzi kana kwamba hawaamini kama kweli mwajuma hatunaye tena duniani.



MWAJUMA IBRAHM SEIF


 


Ulipowasili Mwili huo taratibu za kuutoa zilifanywa na jamaa wa marehemu huku wakifuata taratibu za uwanjani hapo, majonzi na huzuni vilidhihiri watu walipiliona jeneza wani vilio vya hali ya juu vilisikika, aidha mwili huo ulilala kwenye hospitali ya tumbi huko maeneo Kibaha na kuzikwa leo majira ya saa tano na hapo ndio itakuwa safari ya mwisho ya kipenzi chetu Mwajuma.



Marehemu Mwajuma anatarajiwa kuzikwa kwenye shamba lala Dada Yake Mama Warda huko masakuzi Mbezi na misa ya marehemu itafanyikia nyumbani kwa dada yake hapo hapo.


 


Wadau wa bongo5 waliohudhuria kutoka kushoto ni PKJ, Ludokin, Lonely Shirima na Basketmouth
Wadau wa bongo5 waliohudhuria kutoka kushoto ni PKJ, Ludokin, Lonely Shirima na Basketmouth 


 



Kwa taarifa zaidi wasiliana na 0714 581 665.



Mungu ailaze pema peponi roho ya Mwajuma Ibrahim Seif.


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents