Habari

Revolt TV ya Diddy inakuja kuleta kiama cha MTV? Soma uone jinsi walivyojipanga kuleta mapinduzi ya TV

Diddy aliwahi kusema kuwa kamwe hatosimama. Tayari alishauteka ulimwengu wa muziki na sasa anaanda makombora na mizinga kuchukua himaya ya televisheni kwa kile kinachoitwa ‘the biggest network launch in cable history’.

sean-diddy-puff-combs-650-430

Wiki iliyopita Diddy aliingia mkataba na Time Warner Cable ambayo ni wazi itaifanya Revolt TV kuwa channel namba moja ya muziki, nawahurumia MTV.

Actually jana nimekutana na rafiki yangu (kwenye BBALL KITAA ALLSTAR WEEKEND), Gosby ambaye anaifuatilia kwa ukaribu story hii alinisimulia mambo mengi ambayo sikuwa nimeyasoma kuhusu Revolt TV. Story hiyo ilianza baada ya kunikumbusha kuwa Diddy alijibu tweet ya Bongo5 June 21.

Diddy

Gosby alinidokeza kuwa kwa ujio na mikakati ya Diddy na timu yake, MTV waliotawala burudani katika runinga kwa kipindi kirefu wana hali ngumu sana. Hii ni kwasababu Revolt TV inazaliwa katika kipindi ambapo mitandao ya kijamii imekuwa maisha ya kila siku ya binadamu na imechangia kwa kiasi kikubwa kusambaa haraka kwa habari kuliko zamani.

Tazama video hii ‘The Definition of REVOLT TV’ uone walivyojipanga.

“REVOLT is first to be built entirely from the ground up in the social media age,” alisema Diddy kwenye maelezo yake.

Gosby alinidokeza kuwa Diddy na timu yake wanakuja na utaratibu mpya na kuondoa ukiritimba uliopo kwenye TV zingine kubwa katika kupata video za muziki kwa kuitumia pia YouTube ama app maalum ya Revolt kama njia kubwa ya kupata video za muziki duniani.

“REVOLT inaushughulikia utupu kwenye runinga kwa kuwaunganisha wasanii wa dunia, kuwapa nguvu wao na mashabiki wao vifaa na apps kugawa uzoefu halisi wa muziki,” anasema Didy kwenye maelezo yake.

Maana yake ni kwamba kutakuwa na app maalum ya wasanii ambayo itakuwa imeunganishwa moja kwa moja kwenye studio za Revolt na wasanii wanaweza kucontrol matangazo, wanaweza kuweka ratiba ya nyimbo zao wenyewe. Wakati huo kuna app ya watazamaji wenyewe (fan app) ambayo mtu anaweza kubonyeza kitufe cha ‘Go Live’ na kuwa mgeni kwenye kipindi chochote cha Revolt, wanaweza kuhakiki ‘content’ wanayotaka waione hewani, kutengeneza content yao na kuiupload moja kwa moja kwenye kituo cha kituo cha matangazo.

“REVOLT itakuwa jukwaa kwa wasanii wanaochipukia na ambao wana kitu cha kusema. Tutakumbatia muziki halisi, wasanii halisi pasipo siasa zote zilizopo, ” Sean Combs alieleza.

Akiipitisha TV yake Time Warner Cable, hiyo ina maana kuwa Revolt TV itakuwa na subscriber zaidi ya milioni 25 itakapoanza tu. Huo ni ufunguzi mkubwa kama ulivyokuwa wa OWN ya Oprah Winfrey.

Kama Revolt itakuwa na watu milioni 25 waliojiunga, atakuwa na zaidi ya robo ya audience iliyonayo MTV.

“Since MTV stopped playing music videos … it’s left this gaping hole and an opportunity to create not just a network or a channel but an audience company,” he said. “That’s what I like to call Revolt: an audience company that specializes in Millennial. And the number one thing that Millennials like is music, and the number one thing I specialize in is music,” Diddy aliiambia Forbes.

Kwa mikakati hiyo ya Revolt TV, MTV ianze kujipanga upya!! Itaanza matangazo rasmi October 2013.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents