Burudani

Rich Mavoko afunguka baada ya video yake kufikisha views milioni 1

Msanii wa muziki Bongo, Rich Mavoko amefunguka mambo kadhaa mara baada ya video ya ngoma yake ‘Rudi’ kufikisha views milioni moja.

Katika ngoma hiyo muimbaji huyo amemshirikisha Patoranking kutoka Nigeria ambapo siku ya jana ndipo ilifikisha views milioni moja. Akizungumza na The Playlist ya Times Fm Rich Mavoko amesema ngoma hiyo imevunja hata rekodi ya ngoma ya ‘Kokoro’ aliyofanya na Diamond.

“Sometime kuna vitu vingine vinatokea unasema Mwenyenzi Mungu ndio anapanga, hata kipindi natoa Rudi nilitoa tu nikaiweka YouTube audio nikasema acha iende kwa sababu imekaa sana ndani, nikasema kwa sababu watu wameshasikiliza sana audio si rahisi kukimbilia YouTube kuangalia video” amesema.

“Kokoro ilikaa kama wiki tatu ndio ikafikisha milioni moja, kwa hiyo unaona ile mimi nasema ni mabadiliko yametokea, unaona the way watu wanakufuatilia sana” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents