Burudani

Rich Mavoko afunguka kuhusu kuvujisha wimbo wake na Fid Q

Rich Mavoko amepinga tetesi za kuvujisha wimbo aliofanya na Fid Q.

Muimbaji huyo kutoka WCB amesema, yeye hausiki kwenye hilo ila kuna uwezekano hilo lilitokea wakati wa kuamisha kazi hiyo ndipo watu wasio waaminifu walipoipata.

“Sio mimi naweza nikavujisha nyimbo. Fid amenicheck ameniuliza mbona imetoka hivi halafu kule mwisho sisikii ambapo umeimba wewe? Nikamwambia hii ni demo ile ya kwanza,” amesema Rich.

Msanii huyo ameongeza kuwa inabidi wafanye haraka iwezekanavyo kuhakikisha wimbo huo unakamilika ili uweze kuachiwa mara moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents