Burudani

Rich Mavoko amtaja mpenzi wake na kueleza kwanini amedumu naye

Wakati ambapo Fid Q na Nick wa Pili wakidai kuwa ni kosa kubwa kwa staa kumweka hadharani mchumba wake, muimbaji wa ‘Pacha Wangu’ Rich Mavoko ana msimamo tofauti.

1977416_816482978391474_3724788443506466378_n

Akiongea leo kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Mavoko amemtaja mpenzi wake kuwa anaitwa Fey na wamedumu kwa miaka minne sasa.

“Fey ni mwanamke ambaye kwanza nimedumu naye katika mahusiano yetu huu mwaka wa nne pia ambacho nampendea zaidi mpenzi wangu ni kwa kuweza kwanza kuzijua tabia zangu na pia ni mwanamke ambaye anaweza kuniendesha kipindi nikiwa na hasira na nikiwa na furaha, pindi ambapo huwa nipo katika mood mbaya halafu ni mpole na pia ana vitu vingi ambavyo tunaendana mie na yeye,” amesema Mavoko.

Akijibu swali la kama amewahi kumwandikia wimbo Fey, Mavoko alisema:

Unajua mara nyingi sana mie huwa nakaa mtaani na wazee na unajua hicho ndo kinanifanya pia niendelee kuwepo ni kutokana nakukaa na wazee. Unajua huwa wana maneno fulani hivi ambayo huwa yanagusa hasa kwa vijana lakini sikuwahi kuandika nyimbo kutokana na mpenzi wangu ambaye niko naye, kwasababu naishi naye vizuri. Unajua wazee wana maneno sana hasa nikikaa na wazee wakiwa wanacheza bao huwa wana maneno sana kwaHiyo hapo lazima utoke na neno jipya.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents