Burudani

Rich Mavoko atoa sababu ya video ya ‘Pacha Wangu’ kushindwa kuchezwa na TV za nje

Pamoja na kuwa miongoni mwa video bora zilizotoka mwaka jana, ‘Pacha Wangu’ ya Rich Mavoko haijawahi kuchezwa na TV za nje kama zilivyo video za wasanii wengine wa Tanzania akiwemo Diamond, Vanessa Mdee, AY, Alikiba, Ommy Dimpoz, Barakah Da Prince na wengine.

https://www.youtube.com/watch?v=nw59lY5hpF4

“Hii ndio video kubwa niliyowahi kufanya katika muziki wangu,” Mavoko ameiambia Bongo5.

“Ni video ambayo imekuwa na mapokezi mazuri na makubwa. Lakini suala la kwenda kimataifa nafikiri hakuna changamoto yoyote zaidi ya kusema connection ndio kitu muhimu tu. Kila kitu kina wakati wake, ukifika wakati wake wimbo utachezwa, ikifika wakati itaenda tu. Hata kama kuna mtu analeta kikwazo ataachia tu.”

“Ndio maana nikasema mimi nafikiri kila kitu ni wakati, kila mtu ana dream za kuchezwa huko. Wewe jiulize kwanini video nyingine zichezwe kule na hii isichezwe? Sijai kusema kama kuna vikwazo wala kuna mtu labda nina chuki naye, hapana. Hii ni mitihani wakati unataka kufanya kitu lazima ukutane na vikwazo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents