Habari

Richard ajinyakulia $100,000!!!

RichardBaada ya kuishi pamoja ndani ya nyumba ya Big Brother II kwa siku 98, Richard ameibuka kidedea kwa kujinyakulia dola laki moja akifwatiwa na Ofuneka (Nigeria) na mshindi wa tatu ni Tatiana (Angola)
[Angalia video hapa]



Richard


Baada ya kuishi pamoja ndani ya nyumba ya Big Brother II kwa siku 98, Richard ameibuka kidedea kwa kujinyakulia dola laki moja akifwatiwa na Ofuneka (Nigeria) na mshindi wa tatu ni Tatiana (Angola).


Katika matokeo hayo ni kwamba, Richard amechaguliwa na nchi 7, ofuneka nchi 5 na tatiana mshindi wa tatu nchi 1 tu katika fainali iliyofanyika usiku wa kuamkia leo (Novemba 11) Johannesburg Afrika Kusini.


Akiwa katika jumba hilo alijikuta akitumbukia katika dimbwi la mapenzi, kwani alikuwa mshiriki pekee aliyeweka rekodi ya kupigiwa kura ya mapendekezo atoke mara nyingi zaidi.


Kwani mara zote tano alizopigiwa kura aliweza kunusurika, hivyo kusafishiwa njia ya kujitwalia kitita cha dola 100,000 (zaidi ya Sh. milioni 130).


Naye Meneja Uhusiano wa Multi Choice Tanzania Lucy Kiwele aliweza kushangilia ushindi wa Richard hadi kufikia kupoteza sauti alisema Mtanzania huyo anatarajia kurejea nchini Jumatano saa 12:45 jioni kwani ameandaliwa mapokezi makubwa.


Kiwele alisema pia siku ya Ijumaa watamwandalia halfa ‘baab kubwa’ itakayohudhuriwa na wageni waalikwa maalumu (VIP).


Alisema na siku ya Jumapili wataandaa halfa kwa Watanzania wote itakayofanyika katika sehemu maalumu itakayotangazwa baadaye, ili mshindi huyo apate wasaa wa kuwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura zilizomwezesha kushinda.


{iframe width=”260″ height=”365″ frameborder=”0″ scrolling=”no”}http://www.mnetafrica.com/BigBrother/includes/videosmalliframe2.asp{/iframe}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents