Richmond Sasa yaibukia Uganda

Kampuni hewa ya kufua umeme wa dharura, Richmond Development LLC, ya Marekani, limevuka mipaka na kujadiliwa nchini Uganda katika mkutano wa wataalamu wa hali ya hewa, ambao wanasema kwamba Serikali ya Tanzania haikuzingatia ushauri wa wataalamu kwa wakati kabla ya kufanya maamuzi.

Kampuni hewa ya kufua umeme wa dharura, Richmond Development LLC, ya Marekani, limevuka mipaka na kujadiliwa nchini Uganda katika mkutano wa wataalamu wa hali ya hewa, ambao wanasema kwamba Serikali ya Tanzania haikuzingatia ushauri wa wataalamu kwa wakati kabla ya kufanya maamuzi.

 
Ofisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) amelieleza alisema kwamba, sakata hilo limeibuka baada yakusikika kwa taarifa kwamba Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Richmond, ilizingatia taarifa za wataalamu wa hali hewa na ndio maana wakaweza kupata walichokuwa wakikitaka.

 
“Wataalamu na wadau walioshiriki mkutano uliofanyika Entebbe, Uganda, waligusia suala la Richmond kwa kuwa ni wao waliotoa taarifa za mfululizo kuanzia mwaka 2002 wakitahadharisha kuwapo kwa ukame katika maeneo mbalimbali ikiwamo sehemu kubwa ya Tanzania lakini wakashangaa kusikia suala hilo kwa Tanzania lilionekana kuwa la dharura,” alisema ofisa huyo wa masuala ya hali ya hewa Nchini.

 
Katika kamati ya uchunguzi wa wa suala hili, Desemba 5, 2007 ilimhoji Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Mohamed Mhita, ambaye alibainisha wazi kwamba kamati yake imekuwa ikiwasilisha serikalini taarifa zote na baadhi ya taarifa hizo zimekuwa zikinukuliwa vizuri katika vyombo vya habari.

 
Aidha Dk Mahita alielezea wanakopeleka taarifa zao, Dk. Mhita alieleza kamati hiyo kwamba wanapeleka katika idara zote serikalini ikiwa ni pamoja na Ikulu (kupitia Idara ya Usalama wa Taifa), Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Kilimo na pia kupeleka moja kwa moja kwa watumiaji wengine na wananchi kupitia vyombo vya habari.

 
Pia alibainisha pia kwamba mbali ya kuwasilisha taarifa hiyo, wamekuwa wakifanya kazi kwa pamoja katika hatua zote na wataalamu kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu ambao imefahamika kwamba wamekuwa wadau wakubwa wa TMA wakati wote.

 
Ofisa ya mmoja wa TMA alisema kwamba taarifa iliyotolewa na wataalamu Machi 2005 na ile ya Septemba mwaka huo, iliikuta Serikali nzima ikiwa katika joto la Uchaguzi Mkuu huku baadhi ya wataalamu nao wakiwa washiriki wakuu wa harakati hizo kwa namna moja au nyingine ambao walikuwa wametelekeza ofisi zao.

 
“Taarifa tulizozitoa Machi 2005 na ile ya Septemba 2005 zilizoelezea bayana kuwapo kwa upungufu wa mvua katika maeneo mengi ya nchi, ziliwakuta viongozi na watendaji wetu wakiwa busy (katika harakati) za uchaguzi na walipokuja kuzinduka ilikua Februari 2006 wakati mambo yamekwisha kuharibika na hakuna mtu aliyekumbuka taarifa,” alisema.

 
Ofisa huyo ambaye amewahi kushiriki mikutano mingi ya hali ya hewa, alisema kwamba pamoja na udhaifu wao mwingi kiutendaji na kimaadili, rais mstaafu, Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu wake, Frederick Sumaye, walizingatia taarifa za utaribiri za mwaka 2003 na 2004 kwa kutenga fedha na mikakati ya kukabiliana na ukame ulioikumba nchi mwaka 2004.

 
“Mwaka 2004 hata Bwawa la Mtera lilifungwa kwa muda lakini hakukua na mgawo wa umeme na wananchi hawakupata shida ya chakula baada ya Serikali kuwasilisha bungeni maombi ya fedha za ziada ambazo zilitumika kuisaidia Tanesco na Hifadhi ya Taifa ya Chakula (SGR) kwa hiyo Serikali mpya ilijikuta haijajipanga ilipoingia madarakani mwishoni mwa mwaka 2005 na mwanzoni mwa 2006. Nadhani hili ni fundisho kubwa kwetu,” anasema.

 
Katika Mkutano wa Entebbe, pamoja na kutabiriwa kuwapo mvua za wastani katika maeneo mengi ya nchi, bado kuna hatari ya kuwapo uhaba mkubwa wa mvua kutokana na kuwapo kwa mabadiliko makubwa ya joto katika Bahari ya Pacific inayoashiria kuwapo kwa hali ya La Niña, ambayo husababisha upungufu mkubwa wa mvua katika maeneo mengi ya Pembe ya Afrika, Tanzania ikiwamo.

 
Sakata la Richmond lilisababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na mawaziri wengine wawili, waliowahi kuongoza Wizara ya Nishati na Madini iliyoshiriki katika mchakato wa zabuni ya mradi wa Richmond. Mawaziri hao, Dk. Ibrahim Msabaha, ambaye alikwisha kuhamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na aliyechukua nafasi yake, Nazir Karamagi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents