Tupo Nawe

Rick Ross aihama Def Jam na kusaini na Epic Records

Boss wa MMG, rapper Rick Ross ameihama familia ya Def Jam aliyofanya nayo kazi kwa miaka kumi, na kusaini mkataba mpya na label ya Epic Records.

Epic Reords walitoa taarifa hiyo kupitia akaunti yao ya Twitter Jumamosi iliyopita, waliandika “Welcome @rickyrozay to the #EPIC family!”

Katika miaka kumi aliyokuwa na Def Jam, Rozay aliweza kurekodi na kutoa album nane ikiwemo ‘Black Market’ aliyoitoa mwishoni mwa mwaka jana (2015).

Mabadiliko hayo yanamhusu Rozay mwenyewe kama solo, na sio camp yake ya MMG ambao bado wana mkataba na Warner Music.

Rozay anaungana na wasanii wengine aliowakuta Epic Records, akiwemo Future, Diddy, Mariah Carey, Ciara, and Travis Scott pamoja na wengine.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW