Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Rick Ross kutua nchi hii Afrika Mashariki mwezi April, kufanya show ya ‘kukata na shoka’

Rick Ross anatarajiwa kurudi tena Afrika Mashariki kwa mara ya pili kwa ajili ya kufanya show.

Baada ya kutumbuiza kwenye tamasha la Fiesta jijini Dar es Salaam Oktoba mwaka 2012, rapper huyo atatua nchini Kenya kwa ajili ya kufanya show ya kufa mtu.

Tangazo la Ross kutua Kenya, lilitolewa usiku wa jana (Jumatano) wakati wa uzinduzi wa albamu mpya ya Diamond, A Boy From Tandale ambapo sherehe za uzinduzi wake ulifanyika katika ukumbi wa Kenya National Theatre.


Picha ya tangazo la show ya Rick Ross wakati wa uzinduzi wa albamu ya A Boy From Tandale ya Diamond

Boss huyo wa Maybach Music Group anatarajiwa kufanya show hiyo kwenye ukumbi wa Carnivore uliopo mjini Nairobi.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW