Rick Ross mbioni kuingiza sokoni bidhaa kwa ajili ya nywele

Msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani, Rick Ross yupo mbioni kuingiza sokoni bidhaa zake kwa ajili ya nywele.

Rapper huyo anayetamba na ngoma ‘Florida Boy’ aliyoshirikiana na T-Pain na Kodak Black, ameeleza kuwa bidhaa hizo zitaingia sokoni April mwaka huu.

Bidhaa hizo ambazo ni mahususi kwa nywele na ndevu zitajulikana kwa jina la RICHbyRickRoss.

Habari hii njema inakuja zikiwa ni siku chache zimepita tangu kuripotiwa kwa afya ya Rick Ross kuwa mbaya kitu kilichopelekea kulazwa hospitali.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW