BurudaniUncategorized

Rico Single afungua kurasa mpya na video ya wimbo ‘Halindwa’

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva anayefanyia shughuli zake za muziki visiwani Zanzibar, Rico Single, amefungua mwaka 2017 kwa kuachia video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Halindwa’.

Muimbaji huyo ambaye alifunga mwaka 2016 na video ya wimbo ‘Yaani Raha’, amesema mwaka 2017 ni mwaka ambao atafanya mapinduzi makubwa katika muziki wake.

“Kwanza nimeanza na video ya wimbo wangu mpya ‘Halindwa’ ni kazi ambayo kila Mtanzania anatakiwa kuiangalia. Audio ya wimbo imeandaliwa na producer Aloneym kutoka Island Record Zanzibar na video ameandaa na director Ivan na amefanya mambo makubwa sana,” alisema Rico.

Aliongeza, “Kwa mwaka huu bado kuna mambo makubwa yanakuja, hapo ni kama nimefungukua kurasa moja kuna mambo mengine mengi yanakuja, video kali, audio kali mpaka kieleweke,”

Muimbaji huyo ambaye ni mmoja kati ya wasanii wa muziki kutoka Zanzibar ambao wanafanya vizuri, amewataka Watanzania kuipokea kazi yake hiyo mpya.

Katika hatua nyingine, Rico ameweka wazi kwamba, kuimba wimbo wa harakati kama alivyofanya Emmanuel Elibarik (Nay wa Mitego) ni vigumu kwa Zanzibar, kwa madai kwamba mitazamo ni tofauti.

Rico Single alisema siasa visiwani humo ina nafasi kubwa mno na kama msanii atajaribu kuimba wimbo kama huo, huenda akakutana na matatizo makubwa kutoka kwa mtu mmoja mmoja hata kama si mlengwa aliyeimbiwa wimbo huo.

“Huku bana watu wanapenda siasa kuliko fedha, ukiimba harakati kama za wimbo wa Ney utajikuta katika matatizo, maana mtu tu mwenye mapenzi na unayemuimba anaweza kukudhuru kabla hata mlengwa mwenyewe hajakufikia, ndiyo maana harakati huku zimepungua kwa wasanii,’’ alieleza Rico Single.

Rico Single aliongeza kwamba, baadhi ya wasanii wa bongo fleva walishawahi kuimba nyimbo zenye ujumbe wa harakati kwa kuikumbusha serikali mambo maovu yanayofanywa na watu visiwani humo, lakini mapokeo yake yakawa tofauti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents