Habari

Ridhiwan Kikwete awaasa wakazi wa Kinondoni kuhusu Mtulia ‘tunachagua daraja’

Mbunge wa Chalinze kupitia tiketi ya CCM, Ridhiwan Kikwete ni moja ya viongozi waliohudhuria kwenye kampeni za mwisho za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni kumnadi Mgombea wa chama hicho, Maulid Mtulia na kuwaasa wananchi wa jimbo hilo kumchagua Maulid Mtulia.

Mh. Ridhiwani Kikwete akiwa na Waziri wa Tamisemi ,Suleiman Jaffo

Kikwete amesema kuwa wananchi wa Kinondoni wanapaswa kumchagua Mtulia kama kiongozi wao kwani yeye atakuwa daraja kati ya wananchi na Maendeleo.

Kinondoni tunachagua (Maulid Mtulia) Daraja litakayeunganisha wananchi na Maendeleo, #hapakazitu,”ameandika Mhe. Ridhiwan Kikwete kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Marudio ya Uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Kinondoni na Siha unatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi Februari 17, 2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents