Habari

Rihanna ampiga biti Rais Trump kutumia nyimbo zake kwenye shughuli zake za kisiasa

Rihanna ampiga biti Rais Trump kutumia nyimbo zake kwenye shughuli zake za kisiasa

Mwanamuziki Ri Ri ama mwite Rihanna amekuwa ni msanii wa hivi karibuni kuwa na uthubutu wa wa kutamka hadharani na kumtaka rais wa Marekani Donald Trump kuacha mara moja kutumia tungo zake katika mikutano yake ya kisiasa.

Mwanamuziki huyo ajulikanaye kama The Barbadian singer ametishia kuchukua hatua za kisheria baada ya wimbo wake wa mwaka 2008, unaokwenda kwa jina la Don’t Stop the Music, kupigwa katika mkutano wa kisiasa wa raisi Trump huko katika maeneo ya Chattanooga.

Kwa mujibu wa BBC, Rihanna – ajulikanaye pia kama Fenty – timu yake imekwisha tuma barua rasmi katika Ikulu ya Marekani , White House, barua ambayo gazeti maarufu nchini humo Rolling Stone imeishuhudia.

Na inasomeka hivi : “hili limetufikia raisi Trump amekuwa akitumia tungo za muziki za [Rihanna] na rekodi kuu,ikiwemo wimbo wake unaofanya vizuri wa Don’t Stop the Music kuhusiana na matukio kadhaa ya kisiasa uliofanyika nchini Marekani.

“Kama wewe ni lazima au ujue, Bibi Fenty hakutoa idhini yake kwa Mheshimiwa Trump kutumia kazi zake ama muziki wake kutumiwa katika shughuli hizo. Kuendelea kwa matumizi hayo ni tabia isiyofaa.

Miongoni mwa wanamuziki waliothubutu kuzuia kazi zao kutumika katika mikutano ya kampeni za kisiasa , Rihanna anaungana na mamilioni ya wanamuziki hao nchini humo akiwemo Aretha Franklin alizuia wimbo wake wa Amazing Grace wimbo wenye mahadhi ya kidini na baadye ulitumika katika filamu moja baada ya miaka 46.

Matumizi yasiyoidhinishwa ya matumizi ya tungo za mwanamuziki huyo kwenye mikutano ya raisi Trump … inajenga hisia ya uwongo kwamba Bibi Fenty ana uhusiano na, ameshikamana na au kuhusishwa kivingine na Trump.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents