Burudani

Rihanna alivyomfanyia shabiki wake aliyetaka kujiuwa kwa kutoswa

Rihanna amefanya kitu ambacho ni kigumu kwa wasanii wengine kuwafanyia mashabiki zao. Muimbaji huyo ameamua kuoyesha upendo kwa shabiki wake wa kiume ambaye alitaka kujiuwa kutokana na kuachwa na mpenzi wake.

Shabiki huyo anayetumia jina la @WaladShami kwenye mtandao wa Twitter, aliamua kutuma ujumbe wa moja kwa moja kwa Rihanna akimuuliza kuwa alifanyaje mara baada ya kutendwa kwa mara ya kwanza kwenye mahusiano? Na kumueleza kuwa anahangaika sana na hilo.

Lakini Rihanna hakusita kumjibu shabiki wake huyo kwa kumuandikia ujumbe unaosomeka, “Just believe that the heartbreak was a gift in itself! Cry if you have to, but it won’t be forever!” the singer wrote. “You will find love again, and it will be even more beautiful! In the meantime enjoy all that YOU are!!!!.”

Baada ya Walad kupokea ushauri huo kutoka kwa mrembo huyo, aliamua kumshukuru kupitia mtandao huo kwa kuandika, “Thank you, I love you @rihanna.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents