Michezo

Rihanna anataka kununua club kubwa ya soka ya UK, amuomba ushauri Didier Drogba

Rihanna anasemekana kuwa na nia ya dhati kutaka kununua club ya soka ya Uingereza na tayari amezungumza na Didier Drogba ambaye ni rafiki yake wa karibu ili ampe ushauri.

rs_634x1024-140714092235-634.Rihanna-World-Cup-jmd-071414
Rihanna akishangilia kwenye mechi ya kombe la dunia, Brazil

Muimbaji huyo mwenye miaka 26 pia amepanga kuanzisha chuo cha michezo nchini kwao Barbados na kisha anapenda kuwa mwenyekiti ama mmiliki wa club kubwa ya Uingereza. Chanzo kilicho karibu na Rihanna kilidai kuwa awali alidhani muimbaji huyo alikuwa akitania tu kuhusiana na jambo hilo lakini amegundua kuwa yupo serious

Rihanna ni shabiki wa Liverpool. Katika kombe la dunia lililomalizika nchini Brazil, Rihanna alikuwa shabiki mkubwa wa timu mbalimbali zikiwemo Brazil na Ujerumani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents