Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Rihanna na Cardi B ndio wana swagger zangu – Jacqueline Wolper

Msanii wa filamu Bongo na mbunifu wa mavazi, Jacqueline Wolper amefunguka mipango yake katika suala zima la mitindo kuelekea soko la kimataifa.

Akizungumza na Bongo5 amesema moja ya ndoto zake ni kuja kuwavisha wasanii wakubwa Marekani kama Rihanna na Cardi B.

“Rihanna na Cardi B ndio wana swagger zangu kwa hiyo ni watu ambao ninatamani kuwavalisha, na ninajua one day yes,” amesema Wolper.

Katika hilo ameongeza kuwa, “Mitandao inaonyesha na inathibitisha kwamba nimebuni kitu one week akaja akavaa Rihanna, nimebuni kitu one day, kesho yake anakuja anavaa Cardi B,”.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW