Burudani

Rihanna na Shakira kuachia collabo yao ‘Can’t Remember to Forget You’ Jan 13

Uko tayari kwa collabo ya mwaka? Warembo, Rihanna na Shakira wanatarajia kuachia collabo yao iitwayo Can’t Remember to Forget You’ January 13.

shakira-rihanna-crtfy

Rihanna aliweka wazi ujio wa ngoma hiyo kwenye Twitter kwa kuretweet ujumbe wa shabiki uliosema: 14-01-2014 :: @shakira – Can’t Remember To Forget (feat. @rihanna ) na ambapo alijibu: ACTUALLY I just found out you’ll have it by the 13th! #1week.”

Naye Shakira ameonesha kava la wimbo huo kwa kutweet: You guys ready? Jan 13 is almost here. Wimbo huo utakuwa wa kwanza kutoka kwenye albam mpya ya Shakira itakayotoka mapema mwaka huu chini ya RCA/Sony Latin Iberia.

Awali Shakira aliwahi kumshirikisha Beyoncé, kwenye wimbo wao ‘Beautiful Liar’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents