Michezo

Rio Ferdinand atangaza kuhamia kwenye mchezo wa masumbwi (+video)

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand ametangaza rasmi kuingia kwenye mchezo wa masumbwi.

Rio Ferdinand

Rio Ferdinand (38) aliyestaafu soka mwaka 2015 tayari ameanza kuonesha vipande vya video akifanya mazoezi huku akiahidi kuachia  documentary yake kabla ya kuanza pambano lake la kwanza la ubingwa.

Leo mchana Rio Ferdinand anatarajia kuwa na mkutano na Waandishi wa Habari kuelezea nini kimemvutia kuingia kwenye mchezo huo.

Ikumbukwe kuwa Rio ni rafiki wa karibu wa mwanamasumbwi, Antony Joshua na amekuwa akihudhuria kwenye kila pambano lake.

Kwa sasa Rio anajifua na mazoezi kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza chini ya mwalimu wake, Mel Deane mchezaji wa za zamani wa rugby, Tazama baadhi ya video zikimuonesha Rio akiwa mazoezini

https://youtu.be/e-DxQUiWxKg

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents