Burudani

RIP Gregory Isaacs

 

Mwanamuziki mkongwe wa Reggae anayetoka Jamaica, Gregory Anthony Isaacs amefariki dunia tarehe 25 Oct 2010 nyumbani kwake jijini London, Uingereza akiwa na miaka 59.

Gregory a.k.a The Cool Ruler alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya mapafu. Msanii huyo alitamba sana enzi zake kwa miondoko ya Loversrock na mashabiki wengi wa muziki wa reggae wanamtambua zaidi kupitia wimbo wake wa ‘Night Nurse’ aliyoutoa mwaka 1982. Baadhi ya track zake nyingine ni kama ile ya Cool Down The Pace na Stranger in Town.

Katika maisha yake kimuziki, alifanikiwa kutoa albamu zaidi ya 50 ikiwemo ile ya mwisho iliyotoka 2008 ikiwa na jina la ‘Brand New Mimi’.

Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents