AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

RIPOTI: Ariana Grande na Pete Davidson ni wapenzi

Mapenzi kama daladala ukishuka mwenzako anakaa. Ariana Grande anadaiwa kuwa na mpenzi mpya ambaye ni muigizaji na mchekeshaji, Pete Davidson.

Kwa mujibu wa mtandao wa People, umesema mahusiano hayo bado ni mapya kwa sababu ndio kwanza yamenza.

Wawili hao wameingia kwenye mahusiano hayo baada ya kila mmoja kuachana na ana mpenzi wake hivi karibuni. Ariana aliachana na ex wake Mac Miller wakati Davidson alivunja uhusiano na Cazzie David mapema mwezi uliopita.


Ariana Grande akiwa na Pete Davidson kwenye SNL mwaka 2016

Imedaiwa kuwa Ariana na Davidson ambao wote wana umri sawa, walikutana kwa mara ya kanza mwaka 2016 wakati Grande alipokuwa mtangazaji wa kipindi cha Saturday Night Live.

Ariana ambaye alitumbuiza kwenye sherehe za utoaji wa tuzo za Billboard Music Awards Jumapili hii anatarajia kuachia albamu yake ya nne ‘Sweetener’ Julai 20 mwaka huu.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW