Habari

RIPOTI: China kuipiga Marekani muda wowote, bajeti kubwa kupata kutokea yaongezwa

Kuna uwezekano kuwa jeshi la China linafanya mazoezi ya kushambulia vituo vya Marekani na washirika wake huko Pacific hii ni kwa mujibu wa makao makuu ya ulinzi ya Marekani.

Ripoti ya kila mwaka ya Congress inasema kuwa China inaongeza uwezo wake wa kupeleka ndege za kivita kwenye visiwa vyake vya baharini.

Ripoti hiyo inazungumzia kuongezeka uwezo wa kijeshi wa China ikiwemo bajeti kubwa ya dola bilioni 190, thuluthi ya ile ya Marekani. China bado hijazungumzia ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa BBC, Onyo kuhusu mashambulizi ya angani ni moja ya malengo ya kijeshi na kiuchumi ya China.

“Kwa miaka mitatua iliyopita PLA [People’s Liberation Army] limepanua maeneo yake ya kufanyia mazoezi bahrini, na kupata ujuzi wa maeneo muhimu ya baharini na kuna uwezekazo kuwa linafanya mazoezi kushambulia vituo vya Marekani na vya washirika,” ripoti hiyo ilisema.

Inaendelea kusema kuwa haijulikani ni kipi China inataka kudhibitisha kwa kufanya mazoezi kama hayo.

“PLA huenda linataka kuonyesha kuwa lina uwezo wa kushambulia Marekani na vikosi washirika kwenye kambi za jeshi magharibi mwa bahari ya Pacific ikiwemo Guam,” ripoti hiyo iliongeza.

Ripoti hiyo inasema kuwa China inapanga vikosi vyake “kupigana na kushinda”.

“Lengo na mabadiliko haya ni kubuni kikosi hatari kinachozunguka ambacho kitakuwa nguzu ya oparesheni zake,” kwa mujibu wa ripiti hiyo.

Bajeti ya jeshi la China inatarajiwa kuingezeka hadi dola bilioni 240 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Marekani ina wasi wasi kuhusu kuendelea kukua kwa China huko Pacific ambapo Marekani bado ina ushawishi mkubwa.

Kati maeneo ambapo mvutano upo ni kusini mwa bahari ya China ambalo ni eneo linalodaiwa na China na nchi zingine.

Jeshi la Marekani mra nyingi hujaribi kuonyesha kuwepo uhuru kwa kutumia eneo hilo kwa kupitisha ndege zake kusini mwa bahari ya China.

China imekuwa ikapanua kile kinachoonekana kuwa vituo vya kijeshi kwenye visiwa eneo hilo, na imepeleka ndege zake huko wakati ikifanya mazoezi.

Eneo lingine ni Taiwan, ambalo linatajwa na China kama mkoa wake uliojitenga.

Ripoti hii inaonya kuwa China huenda inapanga mikakati ya kuichukua kwa nguvu Taiwan.

Marekani ilikataa uhusiano wake na Taiwan mwaka 1979 lakini inadumisha ule wa kisiasa na kiusalama hatua ambayo ineighadhabisha China.

Marekani pia inaendelea kudumisha uhusiano wake mkubwa wa kijeshi na Japan ambayo ina tofauti zake na China na pia Ufilipino.

Misukosuko isiyokuwa ya kijeshi inaendelea, China na Marekani zimetangaza ushuru kwa bidha za mwingine.

Related Articles

One Comment

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents