BurudaniUncategorized

RIPOTI: Drake kuhama Nike na bidhaa zake za Jordan kwenda Adidas

Siku zote ukiwa maarufu na jina lako ukiweza kulitumia vizuri utaweza kupata dili nyingi kutoka makampuni mbali mbali, moja likiona haufai basi kuna wengine wanatamani kufanya kazi na wewe, na fursa ni kama kiti cha daladala ya Makumbusho-Posta, akishuka mmoja mwingine anakaa.

Imedaiwa kuwa Drake anampango wa kuhamishia bidhaa zake za brand yake ya Jordan na kupeleka katika kampuni ya Adidas.

Drake ambaye amekuwa akifanya kazi kwa pamoja ya utengenezaji wa bidhaa zake hizo na Nike tangu Disemba 2013, amedaiwa kutokuwa na furaha na ushirika wake wa sasa na Nike na anaangalia njia ya kuondoka ili kupata uwezo zaidi wa ubunifu chini ya kampuni ya adidas.

Endapo Drake atajiunga na Adidas atakuwa ameungana na mastaa wengine kama Pharrell Williams na Kanye West ambaye lisababisha Drizzy apate dili na kampuni ya Nike mwaka 2013.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents