Tupo Nawe

Ripoti kamili ya show aliyopiga Diamond Washington DC Hii Hapa!

Umaarufu wa Diamond haupo Tanzania tu bali hata kwa watanzania wengi waishio nchini Marekani. Weekend hii akiwa na madancer wake, aliangusha show ya nguvu mjini Washington DC, huku mahudhurio yakiwa makubwa utadhani kiingilio kilikuwa bure.
Show ilikuwa ya KiVIP zaidi ambapo watu wa rika mbalimbali, masistatu na watu wengi walijitokea kumshuhudia nyota huyo wa ‘Lala Salama’
Kiingilio kwenye show hiyo kilikuwa ni dola 35 ambazo ni zaidi ya shilingi elfu hamsini hivyo ni rahisi kupata picha alilipwa shilingi ngapi kwa show hiyo.
Haijulikani kama atafanya show kwenye miji mingine tena nchini Marekani, lakini kama akifanya hivyo basi atarudi Tanzania with a bag loaded with the Benjamins!!
Hizi ni baadhi ya picha za show zinazoonesha jinsi Diamond na madansa wake walivyofunika.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW