Uncategorized

Ripoti maalum ya kurasa 488 yatoka, ni ya uchunguzi dhidi ya Urusi kuingilia uchaguzi Marekani

Ripoti ya Mchunguzi Maalum Robert Mueller juu ya dhima ya Urusi kwenye uchaguzi wa 2016 nchini Marekani ilifafanuwa kwa kina jinsi Rais Donald Trump alivyotaka kuusitisha uchunguzi huo na kuzuwia haki kutendeka.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ujerumani, Deutsche Welle, Sasa ripoti hiyo inatajwa kuwapa silaha za kutosha za kisiasa wabunge kutoka chama cha Democrat dhidi ya wenzao wa Republican, ingawa hadi sasa hawajakubaliana namna ya kuzitumia silaha hizo.

Ripoti ya kurasa 488 ya Mueller iliyokusanywa baada ya miezi 22 ya uchunguzi wake ilijenga hoja nzito kwamba Trump alijaribu kuzuwia haki kutendeka, lakini ikajizuwia kuhitimisha endapo alikuwa ametenda tendo la kihalifu, ingawa haikumvuwa lawama moja kwa moja.

Kwenye ripoti hiyo, Mueller alisema kwamba baraza la Congress lina mamlaka ya kuchunguza endapo Trump alivunja sehria, kauli ambayo wajumbe wa Democrat walisema wangeliifanyia kazi. 

Mkuu wa chama hicho  kwenye kamati ya sheria ya bunge, Jerrold Nadler, alisema kuwa Mueller amewasafishia njia kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kibunge dhidi ya Trump. 

Image result for robert mueller report

Tayari bunge hilo limewaita kwa mahojiano mwanasheria mkuu na Mueller mnamo mwezi ujao. 

Sehemu ya ripoti hiyo inaonesha kuwa Rais Trump alitaka kuudhibiti uchunguzi huo na kulazimisha kuondolewa kwa Mueller mwaka 2017. 

Ripoti hiyo iliyotolewa Alhamis (Aprili 18) inachambua matukio 10 yanayoashiria uzuwiaji wa haki kutendeka, ikiwemo hatua ya Trump kumfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi, James Comey. 

Mawakili wa Trump wameiita ripoti hiyo kuwa ushindi wa wazi kwa rais huyo. 

Je, Trump kuondolewa kabla ya muda kwisha?

USA PK Justizminister Barr zum Mueller Report (Reuters/J. Ernst)
Mwanasheria Mkuu wa Marekani, William Barr, akijadili ripoti ya Mchunguzi Maalum Robert Mueller na waandishi wa habari

Mjumbe mwengine, Alexandria Ocasio-Cortez, aliapa kwamba angelimuandama Rais Trump kikamilifu kutokana na yale yaliogunduliwa na Mueller, ingawa viongozi wa chama chake walionekana kuondolea mbali uwezekano wa kura ya kutokuwa na imani na rais huyo ukiwa umesalia mwaka mmoja na nusu kabla ya uchaguzi.

“Wengi wanajuwa sipendi sana masuala ya kura ya kutokuwa na imani. Sikulipigia kampeni hilo na nadra kulijadili. Lakini ripoti hii ya Mueller inalileta hilo kizingitini petu sasa,” aliandika mwanasiasa huyo kijana.

Naye Doug Collins, mjumbe wa baraza la wawakilishi kupitia Republican aliandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba kuna mkanganyiko. “Hili si suala la tafsiri ya kisheria, ni usomaji wa insha. Ripoti haisemi kuwa baraza la Congress lifanye uchunguzi sasa juu ya kuzuiwa kwa haki kutendeka. Inasema Congress inaweza kutunga sheria dhidi ya uzuwiaji wa haki kwa mamlaka yake ya Kifungu Nambari 1.”

USA Mueller Report (picture-alliance/AP Photo/J. Elswick)

Mengi ya yaliyogunduliwa kwenye ripoti hiyo yanaweza kutumika kwenye kampeni ya Democrat dhidi ya kuchaguliwa tena kwa Trump, licha ya kuwa wagombea wa urais wa chama hicho walikuwa na tahadhari katika kulisema hilo moja kwa moja.

Ripoti ya Mueller ilitaja “mafungamano kadhaa” kati ya serikali ya Urusi na timu ya kampeni ya Trump na kusema kwamba timu hiyo “ilikuwa na mategemeo ya kufaidika kutokana na taarifa zilizoibwa na kutolewa kupitia juhudi za Urusi,” ikimaanisha kudukuliwa kwa barua-pepe za Democrat.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents