Burudani

Ripoti: Mapacha wa Beyonce na Jay Z walizaliwa kabla ya muda

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umedai kuwa watoto mapacha wa Beyonce na Jay Z waliozaliwa wiki iliyopita walizaliwa kabla ya wakati (njiti).

Ripoti hiyo inasema mimba hiyo ya Queen Bey haikufikisha muda muafaka ni kitu ambacho kimemlazimu kuendelea kubakia hospitalini na watoto wake mpaka sasa tangu alipojifungua Jumatatu ya Juni 12.

Mpaka sasa wazazi hao hawajatoa taarifa yoyote kuhusu kupata watoto hao japo siku chache zilizopita baba mzazi wa Beyonce, Mathew Knowles alisambaza ujumbe mitandaoni akisherehekea kuzaliwa kwa watoto hao.

Mapacha hao wanaongeza familia ya Carter na kuungana na dada yao Blue Ivy mwenye miaka mitano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents