Burudani

Ripoti: Mfumo wa uongozi WCB, mikataba ya wasanii pamoja na wanaomiliki hisa nyingi za kampuni (Video)

WCB ni moja kati ya label kubwa za muziki nchini Tanzania yenye mafanikio zaidi kutokana na ukubwa wa wasanii wake pamoja na uwekezaji walioufanya kwenye tasnia ya muziki wa BongoFleva.

Label hiyo inaongozwa na rais wa label hiyo ambaye pia ni msanii, Diamond Platnumz akishirikiana na Manangers,Sallam aka Mendez, Said Fella maarufu kama Mkubwa Fella pamoja na Hamisi Taletale aka Babu Tale.

Ukiachana na viongozi hao watatu pia kuna mameneja wengine wadogo wadogo ambao wana majukumu ya kuwasimamia wasanii waliosainiwa na label hiyo, ambao ni Ricardo Momo, Makame pamoja Sandra.

Label hiyo ina wasanii saba, Rayvanny, Queen Darleen, Harmonize, Lava Lava, Mbosso, Diamond Platnumz pamoja Rich Mavoko ambaye amekua yupo kimya kwa muda mrefu huku akihusishwa na kutaka kuachana na label hiyo.

Diamond ni nani WCB na wanahisa wengine wa label hiyo.

Diamond Platnumz ndio kila kitu ndani ya WCB, ni Mkurugenzi Mkuu na ndio mwenye hisa nyingi ndani ya kampuni hiyo, hivyo basi ndio mwenye kauli ya mwisho katika maamuzi. Wakurungezi wengine wenye hisa ni pamoja na Sallam, Mkubwa Fella, Babu Tale pamoja na Mama Diamond ambao wanatambuliwa na memorandum ya kampuni hiyo.

Diamond Platnumz

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika kimedai, Mama Diamond yupo kwenye kampuni hiyo kama mkurugenzi huru ambaye ana jukumu la kuangalia kampuni inaendaje pamoja na kutoa ushauri katika baadhi ya mambo.

Kampuni ya WCB yenye makazi yake Mbezi jijini Dar es salaam, kwa sasa inamiliki Wasafi TV, Wasafi Redio,Wasafi.com, Wasafi Records Music Studio, Chibu Perfume pamoja na Diamond Karanga.

Mwaka mmoja uliopita wakati anatambulishwa Mbosso, Fella alitoa kauli ya kumtaka rais wa label hiyo Diamond Platnumz kuongeza kamisheni kwa mameneja hao kutokana na kazi kubwa wanazifanya.

“Kwa mara ya kwanza Diamond ameleta mapindunzi kwenye muziki kwa mameneja kulipwa. Wasanii wengine sisi ndio tunatoa hela, lakini huyu sisi anatulipa, Sallam analipwa japokuwa anauza magari, mimi diwani nalipwa na Diamond, Tale ana ishu zake nyingine lakini analipwa na huyu, na kuna deal nyingine inakuja tutakaa nusu kwa nusu,” alisema Mkubwa Fella

Fella aliwahi kunukuliwa na chombo kimoja cha habari nchini Tanzania  akisema kwamba katika kila mapato ya Diamond ya mwezi mmoja, asilimia 30 inaenda kwa mameneja wake hao watatu. Yaani kama Diamond akiingiza milioni 100 kwa mwezi basi milioni 30 zinaenda kwa mameneja wake.

Fella ana jukumu gani WCB?.
Mkubwa Fella ni mmoja kati ya wakurugenzi wa WCB, lakini pia ana simama kama mmoja kati ya mameneja watatu wa Diamond Platnumz.

Mkubwa Fella

“Mimi ni mmoja kati ya wakurungezi wa WCB lakini pia ni meneja wa Diamond, na kama unavyojua kazi ya mkurungezi wa kampuni ni kuhakikisha kampuni inaenda mbele na inaendelea kukua. Pia kusimamia utendaji mzima wa WCB, kuwaangalia wasanii wetu pamoja na mameneja wao,” Fella aliiambia Bongo5.

Pia Fella ni mzee wa busara ndani ya label hiyo, na mara nyingi ndiye mtu ambaye ana zima moto kama kuna jambo limetokea ndani ya kampuni hiyo. Yeye hufanya hivyo hata nje ya kampuni kama kuna suala ambalo limeleta taharuki huwa anaweka mambo sawa kwani sio mtu wakupaniki na kukurupuka.

Sallam SK ana majukumu gani WCB?.
Sallam aka Mendez ni mmoja kati ya Wakurungezi wa WCB ambaye pia ni meneja wa Diamond wa Kimataifa. Meneja huyo amekuwa akionekana sana katika kumtafutia deals Diamond, shows za nje pamoja na kuingia mikataba na makampuni mbalimbali ya muziki duniani kwa ajili ya kuipeleka kimataifa brand ya WCB.

Sallam SK

Kifesi ambaye alikuwa mpiga picha wa Diamond na WCB, aliiambia Bongo5 kwamba Sallam ni kiongozi wa kampuni hiyo ambaye amechukua jukumu kubwa la kulinda brand pamoja na kuhakikisha kazi za kampuni hiyo zinaenda kama zilivyopangwa.

Babu Tale ana majukumu gani WCB?
Huyu ni Master in Street Management kama anavyojiita mwenyewe. Babu Tale ndiye mwenye kitengo cha lawama WCB lakini ni mlezi wa wasanii pamoja na WCB nzima. Mara nyingi amekuwa mtatuzi wa shida nyingi za wafanyakazi wake lakini ni mtu mwenye maamuzi ya hapo hapo akiona kuna tatizo au kuna mtu analeta shida ndio maana hata baadhi ya wafanyakazi wanaotoka WCB mara nyingi wanamtupia lawama.

Babu Tale

Tale ndiye aliyekabidhiwa kitengo cha lawama kama nilivyozungumza hapo awali, unakumbuka alivyojilipua kwa kauli yake ya kutaka ngoma zao zisipigwe katika vituo vya redio na TV, nani ungeweza kujilipua na kutamba kama alivyofanya Babu Tele?.

Wiki hii aliyekuwa mfanyakazi wa Social Media WCB, Almasi Zambele alidai alitimuliwa WCB na Tale kwa madai bosi huyo alikuwa anahitaji kuweka watu wake wapya. Kama nilivyosema hapo awali, Tale ni mkurugenzi, hawezi kubali mtu achafue brand ya WCB ndio maana hata wakati mwingine analaumiwa lakini kiukweli anatekeleza wajibu wake.

Mikataba ya Wasanii wa WCB

Kama unavyojua WCB ni label kubwa nchini Tanzania, Afrika Mashariki pamoja na Afrika kwa sasa, kwa uchunguzi tulioufanya tumegundua wasanii wengi wana mikataba ya muda mrefu tena yenye vipengele ambavyo ukitaka kusaliti kambi lazima ujiulize mara mbili mbili. Lakini wachache wanadaiwa hawana mikataba akiwemo Queen Darleen ambaye ni dada wa Diamond Platnumz.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya WCB, Harmonize na Rich Mavoko wanadaiwa kuwa na mkataba wa miaka 10 na WCB na mtu ambaye atataka kuvunja mkataba atatakiwa kulipa fidia isiyo chini ya tsh milioni 10. Lakini mikataba yao inaweza kubadilika muda wowote kutokana na mafanikio ya wasanii hao. Mikataba ya wasanii wengine imekuwa ni siri kubwa lakini nadhani umepata picha kwamba WCB ni label ya namna gani mpaka sasa.

Wasanii hao wanaingiza pesa kupitia shows na ishu za matangazo, ambapo kampuni huchukua asilimia kadhaa na pesa nyingine huwenda kwa msanii. Pia ishu za production zimebaki kwa WCB, kuanzia video mpaka audio.

Diamond aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari kwamba kuna baadhi ya wasanii kama Harmonize alitumia zaidi ya tsh milioni 100 kwaajili ya kuandaa kazi zake pamoja na kutengeza brand yake.

Hii imetupa picha kwamba WCB sio label ya kawaida, ni lavel za kimatifa, wasanii na wadau wa sanaa wanatakiwa kuanza kutengeza mazingira ya brand za wasanii kama walivyofanya WCB.

Bongo5 tunawapongeza sana WCB kwa mambo makubwa wanayoyafanya, uwekezaji walioufanya kwenye muziki pamoja na kutengeneza sura mpya ndani ya industry ya burudani na muziki wa BongoFleva Tanzania, Afrika Mashariki pamoja na Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents