Habari

RIPOTI: Plate Number za gari iliyomteka MO Dewji zinafanana na za Msumbiji

Ikiwa ni wiki moja imepita tangu Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mo Dewji atekwe na watu wasiojulikana, hatimaye dalili za kumpata kijana huyo tajiri zaidi barani Afrika zimeanza kuoonekana baada ya  Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro kuonesha picha za gari iliyotumika kumteka MO.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo Ijumaa jijini Dar Es Salaam, IGP Sirro ameonesha picha ya gari hiyo yenye Plate Namba za kigeni zilizosomeka (AGX 404 MC).

Plate Number ya Gari iliyomteka Mo Dewji

 

Kwa mujibu wa mtandao maarufu duniani wa kukagua usajili wa magari wa worldlicenseplates Plate Number ya gari hiyo inayodaiwa kumteka Mo Dewji zinafanana na Plate Number za Msumbiji.

File:Mozambique plate 01.jpg
Plate Number ya Msumbiji

Kwenye Plate Number hizo MC inaeleza kuwa magari hayo yanatoka mjini Maputo (Maputo City) Msumbiji.

Hata hivyo, awali wakati IGP Sirro akiongea na Waandishi wa Habari alieleza kuwa kuna baadhi ya wahalifu nchini wanakimbilia Msumbiji baada ya kutekeleza uhalifu Tanzania. Tazama video akizungumzia tukio hilo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents