Tupo Nawe

Ripoti: Ronaldo anaswa akisaka kanisa la kufunga ndoa na mchumba wake

Fowadi matata duniani wa soka anayekipiga katika timu ya Juventus Turin, Cristiano Ronaldo siku ya jumamosi ya tarehe 17/11/2018 aliamua kwenda kutafuta kanisa na mahali pakufanyia harusi yeke.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 na mchumba wake aliyemvisha Pete ya uchumba siku kadhaa zilizopita  Georgina Rodriguez walionekana wakitembelea kanisa la Gran Madre di Dio lililopo jijini Turin, Italia

Mchezaji huyo machachari ameonekana kuwa na furaha na familia yake licha ya kukumbwa na kashfa ya kubaka huko nchini Marekani.

Taarifa za mtandao wa Daily Mail, zinadai huwenda wawili wao wakafunga ndoa ya kifahari nchini humo kabla ya mwaka huu haujamalizika.

 

Tazama picha hapa chini;

 

 

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW