Habari

RIPOTI: Tanzania na Rwanda zatajwa kuwa na viwango vidogo vya rushwa Afrika Mashariki, Nigeria, Kenya na Marekani ufisadi waongezeka


Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2018 iliyotolewa leo Januari 29, 2019 na Shirika la kimataifa la Transparency International, imeonesha kuwa Tanzania na Rwanda ndio nchi zenye viwango vidogo vya vitendo vya rushwa kwa nchi za Afrika Mashariki.

Ripoti hiyo, imeonesha kuwa kisiwa cha Seychelles kimepanda kwa 66% kupambana na rushwa na inakuwa nchi ya kwanza Afrika kuwa na kiwango kidogo cha rushwa ikifuatiwa na nchi ya Botswana 61% na ya tatu ni Cape Verde kwa asilimia 57 .

Kwa upande wa Afrika Mashariki, Rwanda imekuwa ya kwanza kwa kiwango kidogo cha rushwa na kwa dunia nzima imeshika nafasi ya 48, ikifuatiwa na Tanzania ambayo duniani imekuwa nafasi ya 99 kati ya nchi 188.

Nafasi ya tatu Afrika Mashariki imeshikwa na Kenya, ikifuatia Uganda na Burundi .

Kwa takwimu za nchi zote 188, Denmark imeshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na New Zealand na Finland.

Kwenye ripoti hiyo iliyohusisha nchi 188, imeonesha nchi za Afrika ndio zimeongoza kuwa na vitendo vya rushwa, ambapo kwenye nchi 10 zilizoshika mkia duniani nchi 5 zinatoka Afrika.

Kwa upande mwingine, Marekani vitendo vya rushwa vimeongezeka kwa mwaka 2018 ukilinganisha na mwaka 2017 .

Marekani imeshika nafasi ya 22 na kutoka kabisa kwenye 20 bora ya nchi zenye viwango vidogo vya rushwa duniani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2011 .

Taasisi hiyo imeeleza kuwa, kuzorota kwa demokrasia duniani kumechangia vitendo vya rushwa kuongezeka .

Soma zaidi kuhusu ripoti hii – https://www.transparency.org/cpi2018?utm_campaign=CPI2018&utm_medium=social

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents