Habari

RIPOTI YA LHRC: Vitendo vya ubakaji na ukatili wa kingono vyashamili Tanzania, Mikoa ya kanda ya ziwa yaongoza

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC) kimetoa Ripoti ya Haki za Binadamu ambayo inaonesha vitendo vya ukatili  wa kimwili kwa watoto na wanawake na ubakaji vimeongezeka nchini Tanzania.

Image

Ripoti hiyo ya kuanzia Januari hadi mwezi Juni mwaka 2019 imetolewa leo Jumanne Agosti 20, 2019 na inaonyesha Tanzania Bara, asilimia 66 ya matukio ya ukatili dhidi ya watoto ni ubakaji wakati ukatili wa kimwili ukiwa asilimia 34.

Akisoma ripoti hiyo mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga amesema wafanyaji wakuu wa ukatili huo ni watu wa karibu wakiwemo wazazi, ndugu, jamaa, majirani na walimu.

Amesema asilimia 38 ya matukio ya ukatili kwa watoto yameripotiwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa huku Kanda ya Nyanda za Juu Kusini hasa Mbeya, Njombe na Iringa ikiwa ni asilimia 32. 

Upande wa Mwanza ulawiti wa watoto unaofanywa na watoto wenzao umeonekana kuwa changamoto katika kata 17 ikiwemo Igofo, Igoma na Nyegezi,” amesema Henga.

Mtafiti wa LHRC, Fundikira Wazambi amesema suluhisho la ukatili huo ni kwa jamii kuongeza ulinzi kwa watoto bila kumwamini yeyote.

Usiseme muda mwingi unatafuta fedha wakati mtoto wako wanaangamia, kama baba anaweza kumbaka mwanae vipi kuhusu jirani? juhudi za kulinda watoto ziongezeke,“amesema Wazambi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents