Siasa

Rita Mlaki Ajitoa UWT Dar

MGOMBEA uenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), mkoani Dar es salaam, Rita Mlaki amejiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho kwa madai kuwa ukabila umepewa kipaumbele.

MGOMBEA uenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), mkoani Dar es salaam, Rita Mlaki amejiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho kwa madai kuwa ukabila umepewa kipaumbele.


Rita, naibu waziri wa zamani katika serikali ya awamu ya tatu, aliwaambia waandishi wa habari kuwa siasa hizo za ukabila zimeikumba CCM kiasi cha wagombea kujinadi kwa kushambulia wale wanaoelezwa kuwa si wakazi wa Dar es salaam.


Mlaki aliondoa jina lake zikiwa zimebakia siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo lakini akasema kuwa bado anaipenda CCM, lakini kampeni zinazofanywa za kukichafua hazimfurahishi hata kidogo.


Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa bunge mjini hapa, Mlaki alisema kuwa amefikia uamuzi huo sio kwa kuogopa ushindani bali ni kutokana mmoja wa wagombea wenzake kusema kuwa yeye si mzawa wa Dar es saalam, hali iliyomfanya aone kuwa kuna ubaguzi.


”Sina kinyongo na chama changu wala viongozi wake… najua ni watiifu na kwamba wanajua katika mchakato huu na mimi nilistahili kwa kuwa nina uwezo wa kuongoza ndio maana wakarudisha jina langu, lakini huyo mgombea mwenzetu anafanya kampeni chafu dhidi yetu ndio maana nimeamua kwa moyo mweupe kujitoa,” alisema Mlaki.


Mbunge huyo wa jimbo la Kawe alisema kuwa ameshamuandiakia barua katibu mkuu wa CCM, Yusufu Makamba kueleza uamuzi huo na kwamba nakala ameipeleka kwa mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete na kwa katibu wa jumuiya hiyo.


Alisema kuwa uamuzi huo ulichukua muda mrefu, lakini alipotafakari kwa kina aliona kuwa hakuna sababu ya kuendelea kulumbana na mtu kwani ikifika wakati kama huo watawagawa wanawake wa mkoa huo, jambo litakalo kigharimu chama.


”Mimi nimekuwa kiongozi katika mkoa huo kwa zaidi ya miaka 15 sasa na hadi leo bado ni mbunge wa jimbo na mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa kwa nini niendelee kulumbana na mtu na kupoteza fedha nyingi kwa ajili ya kampeni, kama ni hivyo afadhali fedha hizo nisaidie wananchi na chama changu kwa kukichangia katika matatizo,” alisema huku akionyesha masikitiko makubwa.


Aliongeza kuwa alipata msituko mkubwa baada ya kusikia jina lake likitajwa kwenye kampeni mbaya wakati yeye alijua kuwa mahali pa kukutana na wajumbe ni katika ukumbi

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents