Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Riyad Mahrez ashindwa kuripoti Leicester dili la kutua Manchester City lahusishwa

Klabu ya Manchester City na Leicester wanakaribia kufikia makubaliano ya kusajiliwa kwa Riyad Mahrez kabla ya mchezaji huyo kurejea katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza.

Mahrez raia wa Algeria hakuripoti ndani ya klabu hiyo hapo jana siku ya Jumatatu wakati wachezaji wenzake wakifanya hivyo baada ya kutoka kwenye mapumziko na majukumu ya timu yake ya taifa.

Hata hivyo mchezaji huyo amehusishwa kurejea na wenzake wiki ijayo wakati meneja wa Leicester, Claude Puel akienda nchini Ufaransa na kikosi kilichopo huku kukiwa na uwezekano mdogo kwa Mahrez kuungana nao kwenye kempu hiyo kama dili la kutua Etihad likikamilika.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW