Michezo

Riyad Mahrez usajili uliyogonga mwamba dakika za mwisho

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amepongeza uongozi wa timu hiyo kufuatia kuachana na mazungumzo ya kunasa saini ya Riyad Mahrez wa klabu ya Leicester.

City iliachana na dili hilo kufuatia Leicester kuhitaji kiasi cha paundi milioni 95 swala ambalo liligonga mwamba.

Uongozi wa Man City, uliandaa kiasi cha paundi milioni 65 ili kumsajili staa huyo wa Algeria kitita ambacho kilikataliwa na Leicester City na hivyo kujitoa katika kinyang’anyiro cha mchezaji huyo hapo jana siku ya Jumatano wakati wa kufungwa kwa dirisha la usajili.

“Nimevutiwa na maamuzi yaliyofikiwa na klabu yangu kuachana na dili hilo, pengine katika kipindi kijacho tuta nunua mchezaji kwa gharama hiyo ya paundi milioni 100 lakini sio kwa wakati huu,”amesema Guardiola.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents