Bongo Movie

Riyama adai hataki kusifiwa akifa, ‘sifa mtu uipate ukiwa hai’

Msanii wa filamu, Riyama Ally, amewataka wasanii wenzake kama wanazo sifa zake ni vyema wakamwagia sifa hizo sasa kuliko kusubiri akiwa amefariki dunia.
Riyama1

Riyama ameiambia Mwanaspoti kuwa yeyote mwenye sifa zake za uigizaji au mambo mengine, basi atumie fursa hiyo wakati akiwa hai tofauti na akifariki dunia kwani hatazisikia.

“Nasema mapema, sitaki kusifiwa nikiwa nimefariki dunia, sifa mtu uipate ukiwa hai kama ni faida au kufurahia mwenyewe ujionee lakini nimeshafumba macho kuna faida gani, sisikii sioni haya ya nini kwangu miye?”alisema Riyama.

Msanii huyo alisema imekuwa tabia kwa baadhi ya wasanii kuleta maigizo katika misiba ya wenzao inapotokea mara nyingi wanapoona kamera za vituo vya televisheni.

“Wakiziona kamera hujipanga kwa ajili ya kuhojiwa na waandishi basi hata kama marehemu alikuwa na ugomvi naye, atajifanya jana kabla ya umauti walikuwa wote na kumwachia usia kama rafiki,” alisema.

Source:Mwanaspoti

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents