Robin van Persie amuokoa kitanzini Moyes, ushindi dhidi ya Olympiakos waamsha matumaini ya mashetani wekundu
Hatimaye wachezaji wa Manchester United jana wamecheza tena kama vijana wa Fergie. Kwa mara ya kwanza tangu David Moyes aanze kukinoa kikosi hicho, United jana imecheza mchezo mkali zaidi na kuwapa ushindi dhidi ya Olympiakos uliowafanya waingie kwenye robo fainali ya ligi ya mabingwa wa Ulaya.
Fergie alikuwepo uwanjani kushuhudia vijana wake
Ni Robin van Persie ndiye aliyemuokoa kitanzini Moyes kwa kupunguza presha ya kutimuliwa iliyokuwa imemfikia shingoni baada ya kupachika mabao matatu ya nguvu na moja likiwa la mkwaju.
Shujaa wa mchezo
Ushindi huo umewapa Manchester United walau pumzi ya kupumzika na kunywa maji kwa raha baada ya Jumapili iliyopita kutandikwa bao 3-0 na Liverpool kwenye ligi kuu ya England.
Pamoja na van Persie kuwa shujaa wa mechi hiyo, Moyes anapaswa pia kumshukuru mlinda mlango wake, David De Gea ambaye aliokoa mipira hatari kutoka kwa David Fuster na Alejandro Dominguez muda mfupi kaba Van Persie kufunga goli la pili.
David De Gea akishangilia ushindi
Pamoja na kufunga magoli matatu, Van Persie aliumia goti na kutolewa nje kwa machela
Moyes, ambaye mustakabali wake ulikuwa matatani, alionekana na tabasamu pana usoni baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa
Valencia akisikiliza maumivu ya jicho baada ya kupigwa kichwa