Michezo

Robinho aijibu Mahakama ya Italia kosa la ubakaji

Kufuatia Mahakama ya nchini Italia kumuhukumu kifungo cha miaka tisa jela straika wazamani wa klabu ya AC Milan na timu ya taifa ya Brazili, Robinho hapo jana siku ya Alhamisi kwa kosa la kushiriki kumbaka mwanadada wa Albania tukio lililofanyika mwaka 2013, mwanasoka huyo aijibu mahakama kupitia mtandao wake wa Instagram.

“Nimeshachukua hatua zote za kisheria kwa ajili ya kujitetea, siku husika kwa namna yoyote kwenye tukio hilo kama ilivyodaiwa na tumekata rufaa kupinga hukumu hiyo”, amesema Robinho.

Mahakama ya Milan imesema kuwa Robinho mwenye umri wa miaka 33, akiwa na vijana watano raia wa Brazili walimbaka dada huyo mwenye umri wa miaka 22, baada ya kumlewesha katika klabu usiku, kutokana na wenzake kutofahamika kesi hiyo imeendelea kumkabili peke yake.

Straika huyo aliachana na AC Milan mwaka 2015 baada ya kuitumikia kwa miaka mitano, wakati wa hukumu hiyo ikitolewa mchezaji huyo hakuwepo mahakamani kwa mujibu wa mwanasheria wake.

Robinho,amewahi kuichezea Real Madrid na Manchester City ambapo kwa sasa anakipiga Atletico Mineiro ya nchini Brazil.

Chanzo kimoja cha sheria nchini Itali kinasema kuwa sta huyo wa Brazili bado anayohaki ya kukata rufaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents