Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Robinho apigwa mvua 9 jela kwa ubakaji

Mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid na Manchester City, Robinho, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela.

Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Brazil, amekumbana na kifungo hiko kutokana na kosa la ubakaji alilomfanyia mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 23 huko mjini Milan mwaka 2013.

Hukumu hiyo imetolewa Alhamisi hii ambapo mchezaji huyo anadaiwa kufanya tukio hilo mnamo January 22 ya mwaka huo wakati alipokuwa akiichezea timu ya AC Milan kwa misimu mitano.

Hii sio mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kupatwa na kesi kama hiyo ya ubakaji, mwaka 2009 alikumbwa na kashfa kama hiyo baada ya kudaiwa kumbaka mwanafunzi wa chuo cha Leeds nchini Uingereza.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW